BREAKING NEWS-MABASI YA MIJINI KUGOMA TENA JUMATATU NCHI NZIMA,MADEREVA WAAPA KUTUMUOGOPA MTU,SOMA HAPA KUJUA
| Katibu Mkuu wa Chama cha Madareva Tanzania (TTDA), Rashid Sahele akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) PICHA NA MAKTABA |
NA KAROLI VINSENT
SIKU moja kupita
baada ya Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta kufanikisha kutuliza Mgomo uliokuwa
unataka kufanywa na Wamiliki wa Magari yaendayo Mikoani (TABOA)kupinga tozo za
Nauli mpya,Baada ya Waziri huyo kufutilia mbali Nauli hiyo mpya iliyotangazwa
na Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA).
Nao pia UMOJA wa Madereva Tanzania (TTDA)
umetangaza mgomo wa Mabasi wa yanayofanya kazi ya kupakia Abiria mijini nchi
nzima kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo kwa madai ya Serikali kupuuza matakwa
yao
Akitangaza Mgomo huo, mda huu,Jijini
Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa TTDA, Rashid Salehe wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
ambapo amesema kitendo cha Waziri wa Kazi na Ajira Gaudentia
Kabaka kupuuza matakwa ya kuonana nao ili wamwelieza madai yao wanayoadai kwa
mda mrefu
Katibu huyo aliyataja Madai hayo ni Kupatiwa Mikataba ya Ajira ya
kulipwa kila mwezi ambapo kwa sasa hawana na Kuanza kulipwa kwa utaratibu wa
Kilomteka kwa saa pamoja na kuwekewa pesa kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii iwadaidie
pindi wanapopata Ajali na ikwemo wakati uzeeni .
Dereva
Salehe ameongeza kuwa uamuzi wa kugoma kuendesha
Mabasi itakuwa chachu ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusikiliza kilio chao cha
Mda mrefu ambacho wanasema Waziri mwenye dhamana ya Kazi kuyapuuza.
Pamoja na hayo amebainisha kuwa kwa sasa wameshawataarifu Madereva wote
nchi nzima kutoendesha Mabasi kuanzia Jumatatu ya wiki Ijayo mpaka pale Mmlaka
husika itakaposikia Kilio chao cha kuwahamulu wamikiliki wa Mabasi
kuwatekelezea madai hayo.
No comments
Post a Comment