SERIKALI YAIPIGIA DEBE KATIBA PENDEKEZWA,WAZIRI SAMIA SEMA HAYA,SOMA HAPA KUJUA
SERIKALI
nchini imeendelea kuipigia debe Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la
Katiba kwa kusema Katiba hiyo ni itakuwa ni mwarubaini wa kero za Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar na kuwataka wananchi waipigire kura ya ndio pindi
itakapofika kwao.Anaandika KAROLI VINSENT endela nayo
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa leo tarehe 23 mwezi wa nne mwaka 2015, Jijini Dar es Salaam na Waziri nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Mhe. Samia Suluhu
Hassan (Pichani)Wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari ambapo amesema katiba
iliyopendekezwa na Bunge Maalum itakuwa mwarubaini wa matatizo ya muungano
kutokana na katiba hiyo kutatua changomoto ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele siku nyingi.
Waziri Samia amezitaja Changamoto
ambazo adai katiba hiyo imezitatua ni Suala la mfumo wa Elimu kwenye Vyuo
vikuu,haki ya kumilikia Ardhi upande wa bara,Rasimali ya mafuta na gesi pamoja
na uwiano wa kulipa Deni la Taifa liliopo sasa .
Bi Samia anasema licha ya Katiba mpya
kuja njia ya kutatua changomoto hizo pia
anasema kwenye katiba hiyo kuna mambo mengi muhimu yamewekwa kwenye Katiba hiyo
na yanayohusu muungano jambo ambalo anadai litaleta maendeleo katika nchini.
Pamoja na hayo Waziri Samia ameendelea
kuwataka watanzania kuisoma Katiba pendekezwa na kuipigia kura ya ndio katiba
hiyo pindi itakapokuja kwao.
No comments
Post a Comment