KUBWA-KAMANDA MBOWE AANZA 'KITIMTIM' CHAKE,SASA KUFAGIA SUMU ZA ZITTO KABWE KANDA YA ZIWA,SOMA HAPA KUJUA
KATIKA kujiimarisha kukamata
dola Oktoba mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Freeman Mbowe, ameanza ziara ya siku sita mikoani, ukiwa ni
mwendelezo wa uzinduzi wa program ya mafunzo kwa viongozi wa chama…Anaandika Pendo Omary…(endelea)
Programu hiyo maarufu kama ‘Fast Truck
Program- (FTP)’, ilizinduliwa kwa ajili ya mafunzo ya uzalendo kwa vijana wa
chama ikiwa ni mwendelezo washughuli ambayo imekuwa ikifanywa tangu Januari
mwaka huu.
Wakati Mbowe akielekea mikoani kwa kazi
hiyo, viongozi waandamizi wa kitaifa nao wametawanyika katika kanda mbalimbali
za kichama, wakiendelea kutoa mafunzo kwa viongozi wao wa serikali za mitaa,
ambayo yalizinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Afisa habari wa Chadema, Tumain Makene,
amekiambia chanzo change kuwa, leo Mbowe ameanza ziara yake wilayani
Nzega-Tabora ambapo atazindua FTP eneo la Ndala kisha atahutubia mkutano wa
hadhara.
Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kundi
laUmoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) linaloundwa na vyama vya Chadema, CUF,
NCCR-Mageuzi na NLD, kesho atakuwa Itirima-Bariadi na kesho kutwa atakuwa
Ukerewe mkoani Mwanza.
Makene amesema “siku inayofuata atakuwa
Bukoba Mjini kisha wilayani Kyerwa huko huko mkoani Kagera. Kote huko atafanya
uzinduzi wa FTP asubuhi na jioni atahutubia mikutano ya hadhara”.
Ameongeza kuwa, katika maeneo yote, Jeshi
la Polisilimealikwa kutoa elimu ya ulinzi shirikishi na polisi jamii. Pia
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nayo imealikwa kutoa elimu
ya kupambana na rushwa hasa wakati huu wa uchaguzi.
Kuhusu programu ya uzinduzi wa mafunzo
ya kukiandaa chama kwenda kushika dola na kuongoza serikali, Makene amesema
“Makamu Mwenyekiti wetu, Prof. Abdallah Safari, atakuwa Korogwe Mjini ambapo
atazindua mafunzo hayo kwa viongozi wa Korogwe mjini na vijiji kisha atahutubia
mkutano wa hadhara.”
Makene amefafanua
kuwa, Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika amezindua mafunzo Bariadi kisha
akaelekea Maswa.
“Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum
Mwalimu, amezindua mafunzo mjini Mbalizi mkoani Mbeya kisha akahutubia mkutano
wa hadhara mjini Njombe,” amesema Makene.
Chanzo ni
Mwahalisi.oline
No comments
Post a Comment