MREMA AJIGEUZA DIKTETA,ANG"ANG"ANIA TLP YAKE,SOMA HAPA KUJUA
AUGUSTINE Lyatonga Mrema – Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
Tanzania Labour (TLP), amesema hang’oki kwenye wadhifa huo licha ya baadhi ya
watu kudai amechoka kiumri.Anaandika Pendo Omary….(endelea).
Badala
yake, Mrema ameamua kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanywa na Mkutano
Mkuu 23 Aprili 2015, katika Hoteli ya Kings Palace iliyopo Sinza jijini Dar es
Salaam, akiwa ndiye mgombea pekee aliyechukua fomu.
Akizungumza na Chanzo changu kwa njia ya
simu, Mrema ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, amesema “mimi nina miaka 71. Rais wa
Nigeria – Mohammadu Buhari aliyechaguliwa juzi-juzi ana miaka 72.
Rais wa Zimbabwe – Robert Mugabe ana miaka 92. Mwenye umri mkubwa mnaniona mimi
tu?”
“Kamati Kuu ya TLP iliyopita iliniteua
kuongoza chama hiki. Pia wazee wa Vunjo wameniteua kuwania ubunge katika jimbo
langu kwenye uchaguzi ujao. Ni kwa sababu wananiamini. Kwani hawakumuona
mwingine? Amehoji Mrema.
Mkutano mkuu wa TLP utachagua viongozi wa ngazi mbalibali za kitaifa,
likiwa ni agizo la ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufuatia malalamiko
yaliyowasilishwa kwake na baadhi ya wanachama wakidai viongozi uongozi wa
kitaifa muda wao ulikoma tangu mwaka jana.
Kwa mujibu wa Mrema, wajumbe 120 kutoka nchini nzima watahudhuria
mkutano huo, atakaoufungua saa 6:00 mchana.
Kuhusu malamiko kwamba amekusanya mamluki
wasio wajumbe kuhudhuria mkutano huo, ili kulinda maslahi yake, Mrema amesema
“kuna watu wanafanya kampeni ya kueneza uongo dhidi yangu na chama change.”
“Wanaoeneza habri hizo chafu ni maadui zangu. Sasa hivi wana kampeni
inayoitwa ‘Delete Mrema na TLP’. Lengo lao ni kuniharibia mimi na TLP,” amedai
Mrema.
Chanzo ni
Mwanahalisi.oline
No comments
Post a Comment