NI MUNGU TU ATAKAYEMUOKOA WAZIRI HUYO,MHARIRI WA MTANZANIA AMKABA KOO JIMBONI KWAKE,SOMA HAPA KUJUA
MHARIRI wa Gazeti la Mtanzania, Khamis Mkotya
ni miongoni mwa makada saba wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaotajwa kumnyima
usingizi mbunge wa sasa wa Chemba (Kondoa Kusini), Juma Nkamia-aliye Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Anaandika
Mwadishi Wetu … (endelea).
Mkotya ambaye bado hajatangaza
nia rasmi, jina lake limevuma kwa kiasi kikubwa jimboni humo na kuzusha hofu
kwa Nkamia ambaye anadaiwa kumjengea chuki.
“Nyota ya
Mkotya inamnyima sana usingizi Nkamia, yaani amefikia mahali hata tunapokuwa
kwenye shughuli za kuripoti vikao vya Bunge mjini Dodoma… Nkamia akipisha na
Mkotya akisalimiwa haitikii.
“Kinachomkera ni
kuona namna Mkotya anavyoungwa mkono na wananchi wa jimbo hilo hadi kufikia
wakati wa kumpigia simu au kumwita kumweleza kero zao wakati akiwa bado sio
mbunge,”anasema mmoja wa wahariri.
Mbali na Mkotya,
wengine wanaotajwa ni Raphael Kilesa, ambaye ni Ofisa Utamaduni wa Wilaya,
Juliana Maghembe- mtumishi wa benki moja jijini Dar es Salaam, Fred Duma, Said
Sambala ambaye ni Diwani wa Kata ya Mondo na wengine.
Jimbo hilo lenye
tarafa nne za Goima, Mondo, Kwamtoro na Farkwa ni kati ya majimbo
yanayokabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo uhaba wa huduma za kijamii kama
vile maji, afya, elimu, miundombinu na migogoro ya ardhi.
Chemba ni moja ya
majimbo tisa yaliyopo Mkoa wa Dodoma ambayo yanaonekana kuwa ngome ya CCM,
kutokana na chama hicho kuungwa mkono zaidi kuliko vyama vya upinzani.
Hata hivyo, Nkamia kupitia
kwa marafiki zake wa karibu amekuwa akikiri kuwa Mkotya anamsumbua na
kwamba hana hofu na wagombea wengine.
Kwa mujibu wa
watu hao, Nkamia hana hofu na wagombea hao kwani walio wengi alishindana nao
katika uchaguzi wa 2010 akawashinda, hivyo anajua udhaifu wao.
Mbunge wa zamani
aliyeangushwa 2010, Pascal Degera naye anatajwa kurudi ulingoni. Mgombea huyo
hana madhara kwani licha ya umri wake kuwa mkubwa lakini amekuwa mbunge wa
jimbo hilo kwa vipindi vinne mfululizo (miaka 20), hivyo anaonekana hana jipya.
Upepo wa kisiasa kwa Nkamia unamvumia vibaya, kwani jimboni kwake
malalamiko ya wananchi ni mengi dhidi yake.
Moja ya vitu
vinavyomtafuna Nkamia ni ahadi alizotoa wakati wa kampeni za mwaka 2010.
Anadaiwa kuwa na ahadi nyingi ambazo ameshindwa kuzitekeleza.
Mbali ya ahadi, suala la tabia na kauli za kukarahisha wapigakura
wake ni miongoni mwa vitu vinavyomuweka katika wakati mgumu.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba mwaka jana, ni
moja ya kielelezo kilichodhihirisha kuwa mbunge huyo amechuja, baada ya vyama
vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuzoa vijiji vingi
wilayani Chemba.
Katika uchaguzi huo, vyama vya upinzani vimechukua vijiji 27 na
vitongoji zaidi ya 102 katika jimbo hilo kutoka vijiji 12 walivyokuwa navyo
hapo awali.
Wakati wa kampeni za
uchaguzi huo, Nkamia kama mbunge wa jimbo alishiriki kupanda majukwaani
kuwanadai wagombea wa CCM, lakini jambo la kushangaza katika vijiji vyote
alivyokwenda CCM imeshindwa.
Nkamia mbali ya
kuwa mbunge na naibu waziri, vile vile ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
(NEC) na Kamanda wa Vijana wa Wilaya
Chanzo ni
Gazeti la Mwanahalisi.online
No comments
Post a Comment