HABARI KUBWA.WAZIRI WASIRA AWATIMUA VIGOGO,NI WA MAMLAKA YA RUBADA,WAMEIBA BILIONI 2.5,WAJILIPA POSHO HOVYO HOVYO SOMA HAPA KUJUA

WAZIRI wa
kilimo, Chakula na Ushirika Steven Wasira (pichani)amewafukuza Kazi wakurugenzi
watendaji wa Mamlaka ya Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (Yaani Rufiji River Basin Development Authority – RUBADA) kutokana na matumizi mabaya ya ofisi ya Umma
ambayo yameitia hasara Serikali zaidi ya Bilioni 2.5.Aripoti KAROLI VINSENT
endelea nayo.
Wakurugenzi hao walifukuzwa ni Kaimu
mkurugenzi wa shirika hilo Bwana Alocy Masanja wengine ni mkurugenzi wa Fedha Bwana Filozi John Mayayi pamoja na Mkurugenzi wa Mipango wa shirika hilo Bibi Tabu Ndatulu .
Waziri
Wasira ametangaza uamuzi huo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na
Vyombo mbalimbali vya Habari ambapo amesema
baada ya Ofisi yake kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa vijiji vya Rufiji pamoja na wawekezaji juu ya
Urasimu wa shirika hilo ikiwemo kuchukua
fedha na kutowapatia Viwanja ndipo akaunda timu ya Uchunguzi kutoka wizara ya
Kilimo na Hazina kwenda kuchunguza malalamiko hayo.
“Baada ya kuunda tume ofisini kutoka
hapa Wizarani na kushirikiana na Hazina kwenda kwenye Mamlaka ya Rubada kupitia
hati ya za risiti,tukabaini kwamba mfumo wa pale ni mbovu,ikiwemo wa kukusanya
Fedha,kwani wakawa wanakusanya wenyewe wakurugenzi fedha kwa wananchi na sio
wahasibu wa Mamlaka hiyo,yaani wakawa wanafanya maksudi tu ili kujiwekea mianya
ya kuiba Fedha”
“ Yaani
wakawa wanatumia fedha kwa manufaa yao na sio kupeleka kwenye miradi,hata pesa
zenyewe walikuwa wanakusanya wakawa wanatembea nazo”amesema Waziri Wasira.
Waziri Wasira ameongeza kuwa katika
uchunguzi huo kamati hiyo pia ikabaini shilingi bilioni 2.9 zilizokusanywa kwenye Mamlaka ya Rubada, 715 milioni ndio zilizotumia kwenye
miradi ya Wananchi tu lakini Bilioni 2.5
zimeonekana kwamba zimeibiwa na yaani hazionekani zilipo.
Waziri Wassira alibainisha kuwa mbali
ya kuiba pesa hizo kamati ikabaini kwamba watendaji hao wametumia zaidi ya
Milioni 314 kwenye matumizi ya kawaida ambapo anasema matumizi hayo ni makubwa
zaidi ikiwemo pesa za zilizotengwa na maendelea ya miradi ya Mamlaka hilo
zimepelekwa kwenye mipango ambayo anadai sio ya maendeleo.
Vilevile
Waziri Wassira amesema hata pesa ambazo wamewakata wafanyakazi kwa ajili ya
kupelekwa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii zimekuwa zikiliwa na watendaji hao
tena kwa makusudi pasipo kupelekwa huko.
Aidha,Waziri Wasira amesema baada ya
kupata Ripoti ya Tume hiyo ameiagiza Bodi ya Mamlaka ya Rudaba kuwafukuza kama
mara moja watendaji hao watatu na nafasi zako kujazwa mara moja huku, wakati
taratibu na sheria za kuwafikisha mahakamani zikiwa zinafuata.
Mamlaka ya Rubada ambalo lipo wenye Bonde
la mto Lufiji ambapo kazi yake ilikuwa ni wakuhudumia wananchi wanaotumia
huduma za Bonde hilo.
.jpg)
pichani). Katikati ni Katibu Mkuu Bibi Sophia Kaduma (katikati), na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Dkt. Yamungu Kayandabila
.jpg)
pichani). Katikati ni Katibu Mkuu Bibi Sophia Kaduma (katikati), na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Dkt. Yamungu Kayandabila
No comments
Post a Comment