HABARI KUBWA,ASKOFU GWAJIMA AMELITISA JIJI,WAUMINI WAKE WAMTOA KIJASHO KOVA,APEWA KIBANO KINGINE,SOMA HAPA KUJUA
ASKOFU
wa Kanisa la Ufufua na Uzima Josephat
Gwajima (pichani)amelitikisa Jiji la Dar es Salaam leo mara alipowasili kwenye muendelezo wa
mahojiano na Jeshi la polisi kanda
maalum ya Dar es Salaam ili kujibu tuhuma mbali mbali zinazomkabili,Anaripoti
KAROLI VINSENT endelea nayo.
Askofu Gwajima amewasili leo Kwenye Makao
Makuu ya Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Majira ya saa mbili
kamili asubuhi huku akisindikizwa na viongozi mbali mbali wa Kanisa la Ufufuo na Uzama pamoja na Mwanasheria wake huku kituoni hapo kukiwekwa ulinzi makali kutoka
kwa maofisa mbalimbali wa Usalama wa Taifa na wakisaidiwa na Jeshi la Polisi.
Mara,alipowasili kituoni hapo umati wa Waumini
wake walifulika maeneo yote ya kuingia Kituoni hapo hadi kwenye stendi ya
kupanda Treni ya Reli ya kati waamini hao walikuwa wamekaa huku wakiimba nyimbo
mbalimbali ambazo wanadai zilikuwa zinaimbwa mahususi ili kumpa nguvu Askofu
huyo ajipu kesi hiyo kwa ufasaha.
KUTUKO ASKOFU GWAJIMA KUHOJIWA.
Askofu
Gwajima alitoka kuhojiwa kituoni hapo majira ya saa Saba na nusu mchana huku
bado Afya yake ikiwa sio nzuri ambapo Askofu huyo aligoma kuongea na Vyombo
vya Habari,
Ndipo ikamlazimu Mwanasheria wake Paul Mallya,kuongea na waandishi habari ambapo amesema kwamba mteja wake ambaye ni kiongozi
wakiroho, miongoni mwa mambo aliyohojiwa ni kuhusu mali zake na sio matamshi ya kumtukana
Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam Askofu Pengo.
“Sikilizeni Askofu
kahojiwa maswali mengi tena sio ya kuhusu kumtukana Askofu Pengo maana wametaka
hati ya Helikopta yake anayomiliki,pamoja mpiga wake anayempiga mali zake,Hati
za kanisa alizozianzisha,hati za viwanja vyake hivi ndivo alivyoambiwa apeleke”amesema
Mwanasheria Mallya.
Mallya ameongeza kuwa kutokana na Afya
yake kuzidi chachamaa na kuwa mbaya mahojiano yake yakahairishwa hadi tarehe 19 mwezi huu kwa maojiano mengine.
2 comments
Mwandishi wa habari hii asante kwa taarifa lakini hebu jitahidi uwe unapitia maandishi yako kabla ya kupost manake kuna makosa mengi sana ya kiuchapaji kiasi kwamba ujumbe wako unakuwa hautufikii sawa sawa
Ila imeelewa.
Post a Comment