Zinazobamba

HABARI KUBWA,ASKOFU GWAJIMA AMELITISA JIJI,WAUMINI WAKE WAMTOA KIJASHO KOVA,APEWA KIBANO KINGINE,SOMA HAPA KUJUA


ASKOFU wa  Kanisa la Ufufua na Uzima Josephat Gwajima (pichani)amelitikisa Jiji la Dar es Salaam leo  mara alipowasili kwenye muendelezo wa mahojiano  na Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ili kujibu tuhuma mbali mbali zinazomkabili,Anaripoti KAROLI VINSENT endelea nayo.
     Askofu Gwajima amewasili leo Kwenye Makao Makuu ya Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Majira ya saa mbili kamili asubuhi huku akisindikizwa na viongozi mbali mbali wa Kanisa la Ufufuo na Uzama pamoja na Mwanasheria wake huku kituoni hapo kukiwekwa ulinzi makali kutoka kwa maofisa mbalimbali wa Usalama wa Taifa na wakisaidiwa na Jeshi la Polisi.
           Mara,alipowasili kituoni hapo umati wa Waumini wake walifulika maeneo yote ya kuingia Kituoni hapo hadi kwenye stendi ya kupanda Treni ya Reli ya kati waamini hao walikuwa wamekaa huku wakiimba nyimbo mbalimbali ambazo wanadai zilikuwa zinaimbwa mahususi ili kumpa nguvu Askofu huyo ajipu kesi hiyo kwa ufasaha.
  KUTUKO ASKOFU GWAJIMA KUHOJIWA.
Askofu Gwajima alitoka kuhojiwa kituoni hapo majira ya saa Saba na nusu mchana huku bado Afya yake ikiwa sio nzuri ambapo Askofu huyo aligoma kuongea na Vyombo vya Habari,
         Ndipo ikamlazimu Mwanasheria wake Paul Mallya,kuongea na waandishi habari ambapo amesema kwamba mteja wake ambaye ni kiongozi wakiroho, miongoni mwa mambo aliyohojiwa ni kuhusu mali zake na sio matamshi ya kumtukana Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam Askofu Pengo.
“Sikilizeni Askofu kahojiwa maswali mengi tena sio ya kuhusu kumtukana Askofu Pengo maana wametaka hati ya Helikopta yake anayomiliki,pamoja mpiga wake anayempiga mali zake,Hati za kanisa alizozianzisha,hati za viwanja vyake hivi ndivo alivyoambiwa apeleke”amesema Mwanasheria Mallya.

      Mallya ameongeza kuwa kutokana na Afya yake kuzidi chachamaa na kuwa mbaya mahojiano yake yakahairishwa hadi  tarehe 19 mwezi huu kwa maojiano mengine.

2 comments

Anonymous said...

Mwandishi wa habari hii asante kwa taarifa lakini hebu jitahidi uwe unapitia maandishi yako kabla ya kupost manake kuna makosa mengi sana ya kiuchapaji kiasi kwamba ujumbe wako unakuwa hautufikii sawa sawa

Unknown said...

Ila imeelewa.