HABARI KUBWA.ACT WAMCHIMBA MKWARA KIKWETE, KUHUSU KATIBA,SOMA HAPA KUJUA
![]() |
| Pichani ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Tanzania mama Anna Mughwira. akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mda huu makao makuu ya chama hicho. |
NA KAROLI VINSENT
CHAMA kipya cha siasa cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania) ni kama kimeungana na Vyama vikuu vya
upinzani nchi ambavyo vinaunda UKAWA,baada
ya kusema kitawahamasisha wananchi waipigie kura ya hapana katiba
iliyopendekezwa na Bunge la maalum katiba.
Kwa madai katiba hiyo
imejaa utata ambao unaligawa taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa mda huu Jijini Dar
es Salaam na Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho, Mama Anna Mughwira wakati wa
Mkutano na Vyombo vya Habari kwenye makao makuu ya ACT-Tanzania,ambapo amesema kikao
cha kamati kuu ya chama hicho kilichokutana mwishoni mwa wiki iliyopita walifikia maamuzi
ya kuwataka wananchi kuipigia kura ya hapana katiba iliyopendekezwa.
“Maamuzi ya kamati ya kuu ya chama cha ACT-Tanzania, kwa pamoja tumewataka watanzania
kwa ujumla kuipigia kura ya hapana katiba iliyopendekezwa na Bunge maalum la
Katiba kutokana na katiba hii kutokizi vigezo vyake kwa mtanzania , ikiwemo kutoweka
usawa pamoja kutokuwa tunu za taifa”amesema
Mama Mughwira.
Mama Mughwira ameongeza kuwa Chama
hicho cha ACT-Tanzania kikifanikiwa kuingia madarakani kitahakikisha kinaufuta
kabisa mchako mzima wa kutafuta katiba mpya kutokana na upatikanaje wake wa
sasa kutokuwa na vigezo vya kupata katiba bora.
Kauli ya Chama hicho kipya inaendena na
kauli walioitoa muunganiko wa vyama vikuu vya upinzani ambavyo vinaunda UKAWA
ambao wao kwa pamoja waliwataka wanachama wao kutoipiga kura yeyote inayohusu
kuipitisha katiba iliyopendekezwa.
Mbali na UKAWA pia nalo jukwaa la
kikristo nchini likiwa tayari limetangaza kwa waamini wa dini hiyo kuipigia
kura ya hapana katiba hiyo.
Katika hatua nyingine chama cha
ACT-Tanzania kimesema kinatarajiwa kuanza ziara nchi nzima ambapo ziara hiyo
yenye lengo la kukijenga chama hicho nchi na kusambaza sera zao anazodai ni za
mfumo wa kijamaa.
Aidha,Chama hicho kimezidi kukanusha
vikali tuhuma zinazotolewa kwenye chama hicho ambazo zinasema kwamba chama hicho ni Chama cha
Mapinduzi CCM B,kwa kusema watu wanaosema hivyo wanajenda mbaya na yenye kutakiwa
kupingwa kwani chama hicho kinasera yake
ya mfumo wa ujamaa ambayo wanadai chama cha mapinduzi hakina sera hiyo.

No comments
Post a Comment