BREAKING NEWS-NEC YASALIMU AMRI (BVR) KAULI YA MBOWE YATIMIA SOMA HAPA KUJUA
HATIMAYE
tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)imetanga rasmi kuhairisha kura maoni ya kupigia Katiba
inayopendekezwa na Bunge maalum la Katiba ambayo ilitarajiwa kufanyika tarehe
30 Aprili mwaka huu mpaka pale watakapotangaza tarehe maalum.Anaandika KAROLI VINSENT.endelea
nayo
Kutokana na
Tume hiyo kushindwa kumaliza kuwaandisha kwa wakati wananchi kwenye Daftari la
kudumu la wapiga kura kwa mfumo mpya wa Biometric Voters Regislation,(BVR). nchi nzima kwa mwezi mmoja uliobaki.
Akitangaza kuhairisha zoezi hilo mda
huu jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Jaji Mstaafu
Damiani Lubuva wakati wa Mkutano na vyombo vya Habari ambapo amesema tume hiyo imefikia maamuzi ya kuhairisha kura
ya maoni kutokana na sababu zilizojitokeza kwenye uandikishaji Mkoani njombe.
“Kwa vile zoezi la uboreshaji wa
Daftari la kudumu la mpiga kura halijakamilika,tume haitaweza kuendelea na
zoezi la upigaji kura ya maoni,hivyo zoezi hilo lilitangaza awali la kura ya
maoni kufanyika tarehe 30 aprili limehairishwa hadi tarehe itakayotangazwa na
NEC”amesema Jaji Lubuva
Jaji Lubuva ameongeza kuwa kutangazwa
kwa tarehe husika kutategemea maushauriano na tume ya uchaguzi wa taifa ya
Zanzibar (ZEC).
Aidha,Jaji huyo amesema kuwa kutokana na
uhaba wa vifaa vya kuwaandikisha wananchi kuwa vichache tume hiyo imeshalipia
vifaa vingine ambapo kwa mujibu wa jaji huyo amesema Shehena ya Vifaa
vinatajiwa kuwasili kwa awamu tatu kwaanzia sasa.
“Kwa hali tulioishudia mkoani Njombe
ambapo tulikuwa na mashine 250 kwa sasa tumeona kuagiza vifaa vingi ili tuweze
kuwaandisha wananchi kwa haraka zaidi kwani vifaa vitakuja kwa awamu tano
ambayo kwa sasa zinakuja mashine 268 baadae zitakuja mashine 1600 na ya mwisho
1600”ameendelea kusema Jaji Lubuva’
Jaji lubuva amebainisha kuwa vifaa hivyo
vikija vyote zoezi zima la kuwaandisha wapiga kura litakamilika nchi nzima
mwezi wa Julai.
Vilevile Jaji lubuva amesema kwa sasa
serikali imeshalipa gharaza zote za mashine ambazo anasema zimagharimu Dolla
milioni 72.
Kuhusu kuaomba mashine za BVR nje ya nchi.
Jaji lubuva
amesema ni kweli tume hiyo ilikwenda nchi hizo na kuomba mashine hizo na kudai
hilo ni jambo la kawaida kwani ni nchi rafiki.
Kuibuka huko
kwa tume ya uchaguzi NEC inakuja ikiwa tayari wanasiasa mbalimbali wakiongozwa
na Mwenyekiti wa Chama Demokrasia maendeleo Chadema Freeman Mbowe kupinga zoezi
hilo kwa mfumo wa BVR kusema ni vigumu kufanyika kwa wakati.
No comments
Post a Comment