MAHAKAMA YA KADHI BY BY,SERIKALI YAWAGWAYA MAASKOFU.SOMA HAPA KUJUA
Muswada wa Mahakama ya Kadhi umeondolewa bungeni na sasa
hautajadiliwa katika Mkutano wa 19 wa Bunge unaohitimishwa leo mjini hapa.
Huu ni muswada
wa tatu kuondolewa Bungeni baada ya ile miwili ya sekta ya habari ambayo ni
muswada wa Sheria ya kupata Taarifa wa mwaka 2015 na ule wa sheria ya huduma wa
Vyombo vya Habari iliyoondelewa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Muswada huo
ulipangwa kuwasilishwa Bungeni leo, lakini serikali imeamua kuuondoa kutokana
na hofu ya kutokea mpasuko nchini.
KASHILILA: HAUTAWASILISHWA
Katibu wa Bunge,
Dk. Thomas Kashilila, akizungumza na NIPASHE jana ofisini kwake alisema muswada
wa Mahakama ya Kadhi hautakuwapo tena katika mkutano huo.
Dk. Kashilila
alisema haijulikani ni lini utawasilishwa bungeni kwa sababu Mkutano wa Bunge
ujao unaotarajia kufanyika Mei, utakuwa mahsusi kwa ajili ya bajeti.
“Waziri Mkuu
alivyosema wataangalia na kushauriana kimsingi, alitoa maneno ya busara tu au
ilikuwa kauli ya mtu mzima, lakini huu muswada hautakuwapo,” alisema.
Dk. Kashilila
alisema hali iliyojitokeza Jumapili iliyopita wakati wa semina ya wabunge
haikuwa nzuri kutokana na mvutano mkali miongoni mwa wabunge.
MASAJU AULIZWE SPIKA
Mwanasheria Mkuu
wa Serikali, George Masaju, alipoulizwa kuhusu kama muswada huo utawasilishwa
bungeni, alisema hakuwa na majibu badala yake alitaka suala hilo iulizwe ofisi
ya Spika.
“Suala hili
usiniulize, nenda Ofisi ya Spika au muulize huyu (Magati) ambaye yupo
sekretarieti,” alisema huku akiwa na haraka kuelekea ofisini kwake.
NDUGAI: HAUPO
Naibu Spika, Job
Ndugai, akizungumza na Chanzo changu nje ya ukumbi wa Bunge muda mfupi baada ya
kuahirisha Bunge, alisema muswada wa Mahakama ya Kadhi hautawasilishwa bungeni
leo.
“Huo muswada
hauwezi kuletwa bungeni kutokana na hali ilivyo,” alisema Ndugai bila kufafanua
zaidi.
MIGIRO ANG’AKA
Naye Waziri wa
Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro, alipoulizwa kama muswada huo
utawasilishwa bungeni alimtaka mwandishi asimuulize maswali yanayohusiana na
muswada wa Mahakama ya Kadhi.
“Sitaki kabisa
kuulizwa suala la Muswada wa Mahakama ya Kadhi, kwanza wewe unatoka gazeti
gani, “alijibu Dk. Migiro kwa hasira huku akiingia kantini.
MAASKOFU 4O WAPIGA KAMBI DODOMA
Katika hatua
nyingine, juzi jioni maaskofu zaidi ya 40 kutoka mikoa yote nchini, walikutana
na wabunge katika ukumbi wa Kanisa La Kiinjili la Kilutheli (KKKT) mjini Dodoma
kujadiliana suala la muswada wa Mahakama ya Kadhi.
Baadhi ya wabunge
waliohudhuria mkutano huo waliiambii Chanzo changu kuwa katika mkutano,
maaskofu walitoa azimio kuwa muswada huo usiwasilishwe bungeni kwa kuwa hatua
hiyo inaweza kuhatarisha amani iliyoko nchini.
Maaskofu hao
wanaounda Jukwaa la Kikristo Tanzania, waliwasili mjini Dodoma tangu mwishoni
mwa wiki iliyopita pamoja na mambo mengine kufuatia kama muswada huo
utawasilishwa bungeni.
Hivi karibuni,
Jukwaa la Wakristo Tanzania lilitoa tamko pamoja na mambo mengine kupinga
uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi.
“Ikumbukwe Katiba
Inayopendekezwa ilipitishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba kwa ahadi ya
Serikali kuipa dini ya Kiislam Mahakama ya Kadhi. Inashangaza kuwa hata
Serikali inatoa rushwa ili kufikia malengo yake. Kwa hali kama hii, Kanisa
haliwezi kuunga mkono kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa,” ilisema sehemu ya
tamko hilo.
Kuhusu uanzishwaji
wa Mahakama ya Kadhi , walisema inakiuka misingi ya Taifa kuwa Serikali haina
dini wala mfumo wa sheria unaobagua raia wake kwa misingi ya dini.
Hii ni mara ya
pili muswada wa Mahakama ya Kadhi kuondolewa bungeni saa ya majeruhi kutokana
na upinzani kutoka kwa baadhi ya wabunge.
ULIONDOLEWA FEBRUARI
Februari mwaka
huu, muswada huo pia uliondolewa bungeni kwa kile Mwanasheria Mkuu wa Serikali
alicholiambia NIPASHE kwamba ni kwenda kuonana na viongozi wa dini kuwaelemisha
juu ya mahakama hiyo, ili uwasilishwe tena kwenye mkutano unamalizika leo.
VURUGU SEMINA YA WABUNGE
Mwishoni mwa
wiki nusura wabunge wazipige kavu kavu huku wakirusiana maneno wakati wa semina
kuhusu Mahakama ya Kadhi. Kutokana na joto lilivyopanda, baadhi waliamua
kususia semina hiyo na kutoka huku wengine wakibaki na kurushiana vijembe.
Semina hiyo iliandaliwa na Bunge.
CHANZO: NIPASHE
No comments
Post a Comment