HABARI ILIYOTIKISA JIJI-WAISLAM WAKINUKISHA ,WATOA TAMKO ZITO KUSOMWA KILA MSIKITI NCHINI,SASA WASEMA LIWALO NA LIWE,BOFYA HAPA KUJUA
NA KAROLI VINSENT
SIKU chache
kupita baada ya Mkutano wa 19 wa Bunge
kumalizika,na serikali kuutupia mbali mswaada wa sheria ambao unaruhusu kuwepo
makakama ya Kadhi nchini kutajadiliwa kwenye mkutano huo,
Nayo Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini
wameibuka na kutoa tamko zito kwa kuwataka waislam wote nchini kutoshiriki
kwenye kura ya maoni ya kupitisha katiba pendekezwa Bunge Maalum la Katiba,kwa madai
kwamba serikali haina nia nzuri na waislam nchini kwa kitendo chake cha kukataa
kuwepo mahakama ya Kadhi nchini.Anaaripoti, KAROLI VINSENT,Endelea nayo
Vilevile Taasisi hiyo imewataka pia
waislam wote kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura na
kujiandaa kufanya uamuzi mgumu ambao wanasema hajawai fanywa na waislam nchini
tangu taifa kupata Uhuru.
Akisoma Tamko hilo lenye kura sita jana jioni kwenye msikiti wa Kichangani
uliopo Magomeni Jijini Dar es Salaam ,Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi
ya Kiislam nchini Sheikh Mussa Kundesha kwa niaba ya asasi za kiislam 11
zinazounda umoja huo na kushuhudiwa na Mamia ya waumini wa dini hiyo pamoja
waandishi wa Habari ambapo Sheikh Kundesha alisema-
Waislam wote nchini wamechoka na uonevu
wanaodai kufanyiwa na Serikali iliyoko madarakani kwa kitendo cha kuondo Mswaada
wa Mahakama ya kadhi Bungeni ambapo alisema ni kuendelea kuchochea vita ya
kidini nchini.
“Kuna kila sababu ya kuamini kuwa
Serikali ya CCM imeshindwa kulishughulikia suala la mahakama ya Kadhi katika
uhalisia wake kama ilivyoahidi kupitia ilani yake kwenye uchaguzi ibara ya 108 (b)
mwaka 2005 na sasa inafanya hadaa za kisiasa kuwadanganya waislam ili waonekane
inalishughulikia suala la mahakama ya Kadhi kama walivyoahidi”
“Kwa ubabe
huu wanaotufanyia waislam sasa tunawaomba waumini wote wa kiislam nchini
kutoipigia kura katiba pendekezwa kwasababu sio katiba nzuri kwa waislam harafu
tunawataka kila mmoja aliyetimiza miaka 18 ajiandikishe kwenye Daftari wa
wapiga kura kujiandaa kufanya uamuzi mgumu ambapo utalitikisa nchi”alisema
Sheikh Kundesha.
Alisema kuwa kitendo cha Serikali
kuwatambua Makadhi wa Bakwata pamoja wanachosema ni ‘Mahakama hewa ya Kadhi’
chini ya Bakwata ni kinyume na Katiba ya nchini ibara 19(1) na (20) kwa
kuwalazimisha waislam wawe chini ya Bakwata ambapo wanasema hawatakubaliana
nalo.
KUHUSU TAMKO LA MAASKOFU.
Pia katika Tamko la Taasisi hiyo kiislam ambapo litasomwa kila
msikiti Ijumaa wiki hii nchi nzima pia
wamezungumzia Matamko mawili yaliyotolewa Jukwaa la kikiristo nchini ambapo
Taasisi hiyo ya Kiislam wameonyesha masikitiko yao kwa kusema ni dhahili hapa
nchini kuna serikali dhaifu kwa kuwaacha maaskofu kutoa matamko ambayo wanadai
ni ya kichochezi.
“Ushahidi
kwamba ni chuki tu husda ni pale ambapo hata waislam tuliopendekeza mahakama ya
Kadi iwekwe kwenye Katiba pendekezwa,lakini tunashangaa hawa maaskofu wamekuwa
wakiipinga Mahakama hii wakati hii dini tofauti na y a kwao na sisi waislam
tumewavumilia lakini tunahoji hawa maaskofu wanataka nini”
KUHUSU KESI ZA MASHEIKH NA KUNYIMWA DHAMANA.
Pia Taasisi
ya Kiislam wameonyesha kuchukizwa kwa kitendo cha Masheikh mbalimbali akiwemo
shehe Ponda ambao wapo mahabusu na kunyimwa Dhamana na Serikali ila wanashangaa
kitendo cha Serikali kuwamwachia Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu
Josephat Gwajima wanadai kitendo hicho kinaonesha Serikali kuwapendelea
wakristo.
“Masheikh mbalimbali wako mahabusu wakinyimwa
Dhamana bila sababu za msingi kwa kesi
za uchochezi au kwa kisingizio cha Ugaidi wakati huo huo tumeshuhudia Maaskofu
wakitoa kauli za uchochezi pasina kuchukuliwa hatua yeyote ikiwemo sakata la
Askofu Gwajima”
KAMPENI WANAO DAI KUUA MADRASA.
Pia Taasisi
hiyo wamezungumia kitendo cha Serikali kuwakamata wa Mashehe mbalimbali
wanaowafundisha watoto majumbani kwa madai ya serikali kutofuata taratibu za
mafunzo likiwemo matukioa tofauti yaliyotokea mkoani arusha-
Kwa kusema
ni wazi serikali imejitosa kuua madrasa nchini.
“Lakini
Takriban mwezi mmoja sasa,njama hizi za kuua madrasa zetu zimeibuka kwa kasi
kubwa na nguvu kwa kuendesha kamatakamata ya waalimu wa madrasa zao katika hali
duni majumbani mwao wakifundisha Quran na mafunzo mengine ya Uislam kama
tulivyoshudia huko mkoan Moshi na Arusha”
“Tunataka
Serikali itusaidie kufundisha Elimu ya dini ya Kiislam kwa mujibu wa sheria
ndiyo ipi,sheria hiyo ilipitishwa lini na Bunge lipi?kwa mujibu wa Katiba ya
nchi ibara 20 (1) kazi ya kutangaza dini ni suala binafsi,iweje sasa Serikali
inakuja na madai haya ya kufundisha dini kinyume na Sheria kwa walimu wetu wa
madrasa”
No comments
Post a Comment