BREAKING NEWS-MACHAFUKO AFRIKA YA KUSINI,WAZIRI MEMBE AWAGEUZIA KIBAO WATANZANIA WALIOKO HUKO,SOMA HAPA KUJUA
SERIKALI nchini ni kama imewageuzia kibao watanzania wanaoisha
Afrika ya Kusini baada ya kusema itawarudisha nchini watanzania ambao wamekumbwa tu na machafuko yanayo endelea nchini humo.Anaandika KAROLI VINSENT,endelea nayo
Vilevile Serikali imesema ni watanzania 21 tu ambao ndio wamekubali kurudi nchini kati ya
watanzania 23 waliokimbia machafuko yanayowakumba wageni nchini Afrika ya kusini na kuhifadhiwa
kwenye kiwanja kimoja cha mpira kilichopo nchini humu.
Hayo yabainishwa Mdaa huu Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe
Wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari ambapo amesema Serikali itawarudisha
watanzania ambao wamepata matatizo ya kuvamiwa ambao teyari serikali imeshawatambua,
Na kusema kamwe Serikali haitamrudisha
Mtanzania yeyote ambaye atatumia
machafuko hayo yanayoendelea nchi umo kama njia ya kurudi Tanzania, ambapo
amedai kuwa wapo Watanzania wengi wakihangaika na maisha wakitaka kurudi
nyumbani na kudai kuwa serikali haitoweza kuwarudisha wote kwani wako wengi sana wanaishi huko.
Amebanisha kuwa jambo ambalo serikali inasubili kwa sasa ni kupata
ruhusa kutoka kwa Ubarozi wa Tanzania alioko Afrika ya kusini ili kuwarejesha
watanzania hao waliokubali kurudi
nchini,
Aidha,Katika hatua nyingine Waziri Membe amekanusha Vikali taarifa
zilizokuwa zimeripotiwa kwenye Mitandao ya Kijamii pamoja na baadhi ya magazeti
wakidai kuwa watanzania watatu wamefariki kutoka na machafuko hayo
Ambapo Waziri Membe amesema taarifa
hizo ni za uongo kwani Watanzania hao
watatu wamekufa kutokana na magonjwa mbali mbali na sio sababu ya machafuko
hayo
Membe amewataja watanzania hao ni Athumani China ambaye anasema mtanzania huyo
amekufa kutokana na kupigwa na wananchi wa nchi hiyo baada ya kumpora mwenyeji
wa huko.
Mwingine ni Ally Mohamed ambapo pia amesema huyo naye amefariki kutokana
na kusumbuliwa na ugonjwa wa Kifua kikuu,pamoja na mtanzania mwingine aliyekufa
gerezani alipofungwa ambapo alikufa kutokana na kuchomwa visu.
Vilevile Waziri Membe akawataka
watanzania waishio nje ya nchi kupenda tabia ya kuwa pamoja ili matatizo kama
hayo yaliyotokea Afrika ya kusini ili iwe Raisi kwa Serikali nchi kutoa msaada.
No comments
Post a Comment