HUAWEI YAIPIGA JEKI MICHUANO YA GOFU YA KUMUENZI BETTY MALLABA,SOMA HAPA KUJUA
Mshindi wa Kwanza katika Mchezo huo, Hasnain Rahim (kushoto) akikabidhiwa Kombe na Mkurugenzi wa Mauzo wa Huawei, Samson Majwala.
|
KAMPUNI ya simu
za mkononi ya Huawei Mwishoni mwa wiki iliyopita imefanikiwa kuyadhamini
mashinano ya kumuenzi aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanawake cha Mchezo wa Golf
Tanzania, Betty Malaba aliyefariki Aprili Mosi, 2010.anaandika Mwandishi wetu endelea nayo
Katika
kumuenzi mwanamichezo huyo, nahodha wa timu ya wanawake ya mchezo wa Golf, Hawa
Wanyanche alisema kuwa wameamua kufanya mashindano hayo ili kumuenzi marehemu
Betty aliyeweza kuwaunganisha na timu ya Tanzania kushiriki mchezo wa East and Central
Afrika yaliyofanyika Uganda mwaka 2009 na Tanzania kuibuka washindi chini ya uongozi
wake.
Aidha ,Naye mwanachama wa mchezo huo, Victor
Kimesera alisema kuwa licha ya marehemu Betty kuwa mwanamke, lakini aliweza
kushinda vikwazo vyote vya wanawake katika kujitokeza kuchukua uongozi na pia
uongozi alioweza kuchukua ni wa mchezo wa Golf ambao siyo wa wengi hapa
Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mauzo
na Masoko wa Huawei Tanzania, Samson Majwala alisema kuwa kutokana na kutambua
na kuthamini umuhimu wa mwanamke katika uongozi, hivyo wameamua katika
kumbukumbu ya kumuenzi Marehemu Betty Malaba, kuyadhamini mashindano hayo na
kutoa zawadi aina ya Huawei Ascend Mate 7.
Aliongeza kuwa washindi ambao
wameshinda katika mashindano hayo, wameweza kupata zawadi ya simu, Huawei Ascend
Mate7 mbili, Talk Band pamoja na Router ya Internet ya 4G LTE yenye uwezo wa
kutumia mtandao wa Smile Communication na kuahidi kuendelea kutoa zawadi kwa
vikundi vingine.
Walioibuka washindi katika mashindano yaliyofanyika
katika Viwanja vya Gymkhana, jijinin Dar na kuijinyakulia zawadi mbalimbali ni Hasnain
Rahim, Vikas Varma, Aliasger Mustafa, Ronald Phili na Fatuma Makame.
1.Baadhi ya
wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Huawei wakishikilia simu za
kampuni hiyo.
2.Bango
lenye nembo ya Simu ya Huawei.
3.Sehemu ya baadhi
ya wageni waalikwa.
4.Mkurugenzi
wa Mauzo na Masoko wa Huawei, Samson Majwala akizungumza jambo katika hafla
hiyo.
5.Mkuu wa Kitengo
cha Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Smile, Edgar Mapande (kushoto) na Mkurugenzi
wa Mauzo na Masoko wa Huawei, Samson Majwala pamoja na Victor Kimesera mdau wa
mchezo wa Golf.
6.Majwala
akitoa zawadi kwa mshindi wa mchezo wa Golf.
7.Majwala
akizungumza jambo katika utoaji wa zawadi hizo.
8.Majwala
akionyesha zawadi ya simu ya Huawei Ascend Mate 7.
9.Mshindi wa
mchezo huo (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko
wa Huawei, Samson Majwala.
10.Wahudumu
wa Kampuni ya Simu ya Huawei wakishudia utoaji wa zawadi hizo.
1
No comments
Post a Comment