Zinazobamba

CCM WAANZA KUTIMUANA,WAMFUKUZA MPIGANIA UHURU WA NCHI SOMA HAPA KUJUA

Mwanasiasa Mkongwe nchini na muasissi wa siasa za maridhiano Zanzibar, Nassor Hassan Moyo

MWANASIASA Mkongwe nchini na muasissi wa siasa za maridhiano Zanzibar, Nassor Hassan Moyo, amefukuzwa uanachama wake wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kina mchango wake mkubwa katika kuanzishwa 5 Feb 1977. Anaandika Jabir Idrissa … (endelea).
          Taarifa za kufukuzwa kwake zilipatikana mchana leo na kuthibitishhwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) kupitia taarifa yake ya habari saa moja usiku.
ZBC imenukuu taarifa ya CCM: “Fupi ya CCM Mkoa wa Mjini Magharibi ilitokana na uamuzi wa kikao cha Halmashauri ya mkoa kilichofanyika leo Ofisi Kuu za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar.”
        Taarifa ya CCM haikufafanua sababu za Mzee Moyo kufukuzwa uanachama.
Hatua ya kumfukuza Mzee Moyo inamaana Kamati ya Maridhiano iliyokuwa na wajumbe sita, watatu kutoka CCM na watatu kutoka Chama cha Wananchi CUF, ni shubiri kwa CCM ambayo baadhi ya viongozi wake wakuu wanataka serikali ya umoja wa kitaifa ivunjwe.
Wawakilishi wa CCM katika kamati ya Maridhiano waliokuwa pamoja na Mzee Moyo, tayari walishafukuzwa uanachama, hivyo tukio la hili linahitimisha kuwamaliza wanachama hao walioleta maridhiano wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
           Waliokuwa na Mzee Moyo kwenye Kamati ya Maridhiano ni Mansour Yussuf Himid ambaye alifukuzwa Agosti 2013 na Mohammed (Eddy) Riyami aliyejiondoa mwenzake kufukuzwa.
           Wote sasa wanafanya kazi na CUF kusaidia kampeni ya kupatikana Zanzibar yenye mamlaka kamili.
Mansour ambaye ameteuliwa kuwa katibu wa kamati ya mkakati ya kuhakikisha ushindi wa Maalim Seif Sharrif Hamad, ameshatangaza kugombea uwakilishi jimbo la Kiembesamki.
             Mzee Moyo aliliambia gazeti la MwanaHALISI Online kuwa taarifa hizo amezisikia juu juu tu, kwani hajapewa taarifa rasmi ya kufukuzwa uanachama wake.
“Mimi sipo Zanzibar, taarifa hizo nimezisikia juu juu tu, lakini muda muafaka ukifika nitatoa tamko rasmi,” anasema Mzee Moyo anayemiliki kadi namba saba.
            Mzee Moyo anasema, hashangai kusikia kuwa amefukuzwa kwani mara kadhaa viongozi wa CCM wa mkoa wa Wilaya, walikuwa wanamtaka awarushie kadi yake ya uanachama, lakini aligoma na kuwaambia labda akiitaka Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
               Vuguvugu la kumvua uanachama Mzee Moyo ulianza tangu kamati yake ya Maridhiano ilipofanikisha kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa baada uchaguzi 2010 amekuwa akipigania kuwepo Muungano wa serikali anaosema ndio wa haki na utaipa Zanzibar serikali yenye mamlaka kamili kinyume na ilivyo uhai wote wa Muungano miaka zaidi ya hamsini.
         Msimamo huu unapingana na sera ya CCM inayoshikilia Muungano wa Serikali mbili. Msimamo wake unachukuliwa kama ni msimamo unaoendana na CUF hivyo kuwekwa kundi la kusaliti CCM.

Chanzo ni Mwanahalisi.oline

No comments