NEC YAKUBALI KUSHINDWA,YACHUTAMA RASMI BVR,YALIOSEMWA NA MBOWE YATIMIA SOMA HAPA KUJUA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi
nchini Tanzania (NEC) imesema inawasiwasi na zoezi la kura ya maoni ya
kupitisha Katiba inayopendekezwa kuahirishwa kutokana na kusuasua kwa mwenendo
wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapigakura linaloendelea mkoani Njombe.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Mkoani Njombe Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa kura ya maoni ya Katiba mpya inayopendekezwa huenda isifanyike mwishoni mwa mwezi Aprili na kusogezwa mbele ili kukamilisha uandikishwaji wapigakura.

Kusogezwa huko mbele kwa kura ya maoni kutakuwa ni pigo kwa Rais Jakaya Kikwete na Chama chake cha Mapinduzi CCM ambao walikuwa wanafosi kura hiyo ipigwe tarehe 30 April mwaka huu.
Licha ya Rais Kikwete na Chama chake kung'ang'ania kura hiyo lakini viongozi wa upinzania wanaounda UKAWA walikuwa mastari wa mbele kupinga kura hiyo kwa madai uandikishaji kwenye daftari la kupiga kura ulikuwa na dosari nyingi pamoja ulagai wa serikali.
kukwama huko kwa tume ya uchaguzi kunatokana na Serikali kukosa pesa kwa mda huu,uku ikizingatia nchi wahisani wakiongozwa na marekani wakiwa wamegoma kutoa pesa kwenye bajeti ya Tanzania kutoka na serikali kushindwa kutekeleza ipasavyo maamuzi ya Bunge kwenye sakata la Ukwapuaji mabilioni ya shilingi kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.
No comments
Post a Comment