Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO-LOWASSA AWAPONZA WANAFUNZI UDOM,UONGOZI WAANDAA PANGA,WANAFUNZI WENGINE WAWASUTA,SOMA HAPA


UONGOZI wa chuo Kikuu cha Dodoma unaangalia uwezekano wa kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wanafunzi wa chuo hicho walioandamana mpaka nyumbani kwa kada wa chama cha Mapinduzi CCM Edward lowassa kwa kumtaka agombee Urais hapo baadae mwaka huu.Anaandika KAROLI VINSENT endelea.
      Wanafunzi hao wa shahada za juu kutoka chuo hicho waliandamana mwanzoni mwa wiki hii kwenda nyumbani kwa lowassa wakiwa na mabango pamoja pesa  ambazo wanadai wamechangishana na kumpatia Lowassa ili itumike kwenye gharama za kuchukulia fomu ya kutaka nafasi ya Urais ndani ya chama cha mapinduzi CCM.
     Kwa mujibu wa Mtoa taarifa wetu aliyoko kwenye chuo kikuu hicho anasema kwa sasa viongozi wa juu wa chuo hicho wanatafakali na kuangalia ni hatua gani watachukua kwa wanafunzi waliokwenda kwa Lowassa.
       “Kusema kweli wanafunzi hawa wametufedhesha sana kwa utoto huu waliofanya,yaani wamekihaibisha chuo hichi ambacho kinasifika kwa kutoa elimu hapa nchini,na tangu jana walivyoenda huko Makamu mkuu wa chuo hichi amekasirika sana na uwenda akachukua hatua za kinidhamu kwa wanafunzi hawa”kimesema Chanzo chetu.
          Lowassa ambaye aliwai kuwa waziri mkuu ambapo alijiuzulu kutokana na yeye kuhusika kwenye ufisadi mkubwa ambao unalighalimu taifa mpaka leo kwenye Kampuni tata ya kufua umeme ya Richmound ambaye sasa anatajwa ni miongoni mwa makada wa Chama cha Mapinduzi CCM ambao wanaoutaka Urais kwa udi na Uvumba.
        Mtoa taarifa mwengine kutoka chuo hicho ambaye yeye anatoka kwenye ofisi ya taaluma ameuambia mtandao huu kwamba kama chuo makini hakiwezi kufumbia kile anachokiita ni utovu wa ni Nidhamu wa hali ya juu kwa wanafunzi kuacha kusoma na kujiingiza kwenye masuala ya siasa.
          “sisi wenyewe leo tulitegemea labda ofisi ya mawasiliano ya (UDOM) ingetoa Tamko kuhusu hatua ya wanafunzi hawa kwa njaa zao  kuwafuata watu mafisadi,harafu sijui kwanini viongozi,wanaangalia ila nimesikia chuo wanaangalia hatua zipi watachukua maana kama tukiacha kitaonekana chuo ambacho kinazalisha wanasiasa wenye kutafuta pesa na sio wasomi bara wa hizo siasa na masomo mengine”amesema.
          Kuibuka huko kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo hicho kutoa matamko au kufanya mambo yanayooneka ni ya kama ya kisisa yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ikumbukwe kwenye sakata la Ufisadi wa Escrow wanafunzi wa chuo hicho walitoa tamko la kumtaka Rais Kikwete awachukulia hatua viongozi walioingiza nchi kwenye ufisadi huo.
    WANAFUNZI WENZAO WA UDOM WANENA.
Nao baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho waliozungumza na mtandao huu kwa sharti la kutotaja majina yao wala kozi wanazosoma,wameonesha kuchukizwa na kitendo cha wanafunzi wa chuo hicho kwenda kwa Lowassa.
             “Mimi nashangaa sana nchi nzima kunavyuo vikuu vingi sana mbona hatuwaoni kujiingiza kwenye utoto huu,yote haya yanatokana na uongozi wa chuo chetu kuendelea kuuuwafumbia macho wanafunzi hawa ambao wanawaza pesa tu”
          Kwa upande wake mwanafunzi mwengine amesema kwa kufichua mchezo mchafu ambao anadai hata pesa waliomkabidhi Lowassa imetoka kwa makundi la Lowassa.
“Yaani huyu jamaa sijui anang’ang’ania nini huku Ikulu yaani anayekwambia hata hizo pesa ni za kwao hao wanafunzi ni muongo bwana hizo pesa zimetoka kwa mtu bwana Ipson ambaye ni mtu wa lowassa na amempa (anamtaja jina”ndio kiongozi wa chuo hichi ambao wanaapa kumuunga mkono Lowassa”
  WANAFUNZI WA VYUO VINGINE WANENA.
      Kwa upande wao wanafunzi wa vyuo vingine nao hawakuwa nyuma kuzungumzia hatua hiyo ya wanafunzi wenzao wa chuo kikuu cha Dodoma.
  wakwanza alikuwa ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania Israel Mwalenge naye amesoneshwa na kitendo cha wanafunzi hao kwa kusema wanakifedhehesha chuo.

“Hata mimi nashangaa sana,lakini inaonekana uongozi wa chuo hicho hawako makini,hivi wanavyofanya hivyo wanakishusha chuo hicho kikubwa  hapa nchini”amesema Mwalenge. 


WANAFUNZI WENYEWE HAO HAPO WAKIENDA KWA LOWASSA




Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwasalimia mamia ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dodoma, waendesha boda boda na wamachinga wa mkoa huo walioandamana hii leo hadi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma kumuomba pindi wakati ukifika kwa mujibu wa taratibu za chama cha Mapinduzi (CCM) asisite kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais. 

Lowassa amesema anazidi kuhamasika kufuatia maombi ya watu wa makundi mbalimbali ya jamii wanao muomba kugombea urais mwaka huu.

Aidha na yeye amewaomba vijana hao na makundi mengine kuwahimiza wenzao vyuoni na hata mitaani kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili siku ya uchaguzi wawe na sifa za kuweza kushiriki katika uchaguzi kwa kupiga kura. 
 
Rais wa serikali ya wanafunzi akizungumza
Mheshimiwa Lowassa akizungumza na wanachuo hao
 Wanafunzi hao zaidi ya 300 walifika nyumbani kwake hapo majira ya saa sita mchana na kuzungumza nae na kufikisha salamu zao ikiwa ni pamoja na kumchangia fedha za kuchukulia fomu.
Aidha Lowassa kwa Upande wake amewashukuru vijana hao na kusema kuwa ujio wao na ule wa masheikhe wa Bagamoyo unazidi kumhamasisha kutangaza nia na pindi muda ukifika anaweza kufanya hivyo.
 Walibeba na mabango yaliyo na jumbe mbalimbali
 Bodaboda nao walifika eneo hilo
Sehemu tu ya umati uliofika nyumbani hapo kwa Lowassa hii leo.


No comments