HABARI KUBWA-PROFESA BAREGU AMLALUA ZITTO,ASEMA NI MTU WA HOVYO.SOMA HAPA KUJUA
PROFESA Mwesiga Baregu, mmoja wa watu
wanaoheshimika nchini amesema, aliyepata kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto
Kabwe, anaponzwa na kibuli cha kujiona hakuna zaidi ya yeye. Anandika
Saed Kubenea … (endelea).
Amesema, Zitto
ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina
mavuno.
“Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi
za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama
yake mzazi kumlea kijana huyu.”
Kauli ya Baregu
ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na
Chama cha ACT – Tanzania.
Prof. Baregu
aliwahi kuwa “mlezi wa Zitto” ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto
(marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho “kusaidia
kumlea.”
Prof. Baregu ambaye ni mjumbe wa
kamati kuu ya Chadema anasema, “Zitto hamnazo. Amekuwa anajiona yeye ni zaidi
ya chama. Hashauriki.”
Anasema
wakati ule alipopewa kazi ya kumlea Zitto “katikakati ya migogoro, tulikuwa
tunazungumza naye mara kwa mara. Ninamfahamu. Kazi hii ya kumlea tulikabidhiwa
mimi na mama yake mzazi, Bi. Shida Salum,” anaeleza Baregu.
Mama mzazi wa
Zitto, alifariki dunia Juni mwaka jana, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kauli ya Prof. Baregu ilifuatia gazeti hili kutaka maoni yake juu
ya mustakabali wa kisiasa wa Zitto baada ya kuwahi kujiondoa ndani ya Chadema.
Chanzo ni Mwanahalisi.online
No comments
Post a Comment