ZITTO KABWE APIGWA 'STOP' ACT.UROHO WAKE WA MADARAKA WAZIDIMTESA.SOMA HAPA KUJUA
BAADA ya kutimuliwa
Chadema na kukimbilia Chama cha ACT-Tanzania, Zitto ameanza kuwekewa vigingi
akitakiwa kutogombea nafasi yoyote ya uongozi wa kitaifa utakaofanyika 28 Machi
mwaka huu.
Kigingi hicho, kimewekwa na Mwenyekiti wa ACT
aliyesimamishwa uongozi, Kadawi Limbu, akisema Zitto aliyejiunga na chama hicho
siku nne zilizopita anapaswa kusubiri mpaka atakapotimiza miezi sita ya
uwanachama wake.
Limbu ambaye bado
anajitambua kama mwenyekiti halali wa ACT-Tanzania, ametoa tamko hilo wakati wa
mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Mimi bado ndiye
mwanyekiti wa ACT- Tanzania kwa vile barua inayodaiwa kuniondoa katika
nafasi ya uenyekiti haikuwa halali na ilinifanya nipeleke suala hilo mahakamani
kwa ajili ya kupata muongozo,”amesema.
Kwa mujibu wa Limbu,
katiba ya chama hicho inaelekeza wazi kwamba mwanachama yeyote anayetaka
kugombea nafasi ya uongozi ni lazima uwanachama wake uwe umetimiza zaidi ya
miezi sita tangu ajiunge na chama hicho.
“Mkiangalia mtaona
Zitto ambaye amejiunga na chama hicho hivi karibuni katika mazingira tata,
katiba haimruhusu kugombea nafasi yeyote katika chama chetu, nimuombe kwamba
andelee kuwa mwanachama wa kawaida tu,”amesema Limbu.
Pia, amemtaka Katibu
Mkuu wa ACT-Tanzania, Samson Mwigamba kuacha kuwapotosha wanachama kuhusu
uchaguzi huo kwani sio wa halali kutokana na Limbu kufungua kesi ya kikatiba
mahakamani kupinga kuondolewa katika nafasi ya uenyekiti.
Akizungumzia chanzo
cha mgogoro huo, Limbu amesema yote hayo yamechangiwa na Ofisi ya Msajili wa
Vyama vya Siasa, kutokana ofisi hiyo kufanya kazi kwa utashi huku ikitoa
taarifa zinazokanganya.
Limbu amefafanua kuwa
ameamua kumpeleka Msajili katika Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru), kwa madai kuwa amekula njama katika kumpa barua ya kumzuia
kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Ametoa angalizo kwamba
atapigana hadi kufa kuliko kuona chama hicho walichokianzisha kwa gharama
kubwa, kikiangukia mikononi mwa mafisadi.
“Kuna watu wanajiita
wazalendo lakini ukiwafuatilia utabaini kuwa wamejivika kofia hiyo kwa ajili ya
kunyang’anya haki za wenzao. Watu hao ni sawa na majambazi,”amesema.
Hata hivyo, uongozi wa
ACT-Tanzania, umesema katiba yao, iliyoko kwa Msajili wa vyama vya siasa,
inaonesha kwamba mwanachama yeyote anaweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi
endapo ametimiza siku saba tangu ajiunge na chama hicho.
Chanzo ni mwanahalisi,online
No comments
Post a Comment