MSANII WEMA SEPETU NA MILLARD AYO WAPAGAWA NA GARI LA MITSUBISHI ASX,SOMA HAPA KUJUA
| Pichani ni gari jipya la mitsubishi ASX likizinduliwa rasmi wiki iliyopita |
| Msanii maarufu nchini Wema sepetu akipanda Gari hilo jipya na la kisasa kabisa |
| Pichani ni Meneja mauzo wa Diamond \ Motors,Reena Ganatra Akizungumza na waandishi wa Habari |
MTANGAZAJI
wa Clauds FM.Miladi Ayo na Mwigazaji maarufu nchini anayesifika kwa mbwembe
mbalimbali,Wema Sepetu wamesifia gari jipya la Mitsubishi ASX la mwaka
2015,linalouzwa na kusambazwa na Kampuni ya Diamond Motors (Hansa
Group)Anaandika KAROLI VINSENT,Endelea nayo.ubishi ASX kabla ya uzinduzi.
Katika uzinduzi wa Kutambulisha
gari hilo,uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,pamoja na mambo mengine
Kampuni ya Diamond Motors wauzaji pekee wa magari kutoka mitsubishi waliwaalika
Milard Ayo na Wema Sepetu kujaribu gari hilo toleo jipya mitsubishi.
Mastaa hao walivutiwa na mwonekano wa
Mitsubishi ASX lenye vioo vya kisasa juu vyenye mwanga unaowezesha dereva
kufurahia mwonekano wa upande zote.
Meneja mauzo wa Diamond Motors,Reena Ganatra
alisema Gari hilo lenye luninga ndogo inayocheza DVD,Ipods,Bluetooth na sauti
kutoka vyanzo mbalimbali ni maalum kwa vijana wa kisasa na Familia kwani Mitsubishi ASX.
limetengenezwa na teknolojia ya MIVEC yenye
kulifanya liwe na nguvu ya 150 ps katika 6,000 rpm na nguvu ya kuzunguka kwa
mwendokasi mkubwa na kwamba limetengenezwa maalum kutumia mafuta madogo.
Meneja huyo ameongeza kuwa injini ya
gari ambayo ni 2.0 liter imeunganishwa INVECS-111CVT inayosaidia mwendelezo
wake katika kubadili mwendo pamoja na uimara wa usukani unaosaidia mikono ya
dereva kuwa salama hata unapokuwa Katika mwendo mkali.
Aidha,Bwana Ganatra alisema kwa sasa
gari hilo litauza kwa dola za kimarekani elfu 28 tu,na litakuwepo kwenye maeneo
mbalimbali hapa nchini.
Vilevile Ganatra akawataka wananchi
kuchangamkia fursa ya kununua magari hilo kwani ni kimbilio kwa watu wenye
kipato cha chini.
No comments
Post a Comment