MPANGO WA KUMUUA DOKTA SLAA WAVUJA,USALAMA WA TAIFA WATAJWA,MARANDO AMVAA MANGULA WA CCM SOMA HAPA KUJUA
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando (kushoto) na Mkurugenzi wa Operesheni ya Uchaguzi wa Chadema, Benson Kigaira |
MABERE Marando- Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama
cha Demokrasia na Madendeleo (Chadema), amefichua mawasiliano ya siri
yanayofanywa na vyombo vya dola dhidi ya chama, na mkakati wa kumdhuru Katibu
Mkuu, Dk. Willibroad Slaa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).
Amesema kuwa Idara ya Usalama wa Taifa
na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philip Mangula, wamekuwa wakimtumia Khalid
Kagenzi-mlinzi binafsi wa Dk. Slaa ili kurekodi na kuvujisha taarifa za vikao
vya siri vya Chadema.
“Kama chama
tumelalamikia sana serikali ya CCM kwa matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi
yetu. Sasa tumebaini wanatumia vijana wetu kunasa taarifa zetu.
“Kagenzi kwa miaka
miwili tumebaini amekuwa akitumika kupeleka taarifa za Chadema kwa usalama wa
taifa. Amekiri hilo kwa maandishi na kutaja namba za watu wa usalama
anaowasiliana nao,” amesema.
Marado alimtuhumu
Mangula kuwa imebainika anawasiliana na Kagenzi ikiwa ni pamoja na kumtumia
fedha mara mbili, Julai 24 na Desemba 4 mwaka jana, kupitia simu yake ya
Vodacom (anaitaja).
Kwa mujibu wa
Marandu, mlinzi huyo alipobanwa zaidi alieleza mkakati uliokuwa ukipangwa na
watu hao wa kumwekea Dk. Slaa sumu kwenye chakula au kinywaji.
Amesema kuwa wamebaini nyendo hizo hivi karibuni baada ya mlinzi
huyo kuonekana akipanda katika gari ya afisa usalama wa mkoa wa Kinondoni lenye
namba za usajili T213 ARS, akiwa nalo afisa msaidizi.
Marando amefafanua kuwa watamfikisha Kagenzi polisi ili achunguzwe
na hatua zaidi zichukulie, lakini akakataa kuweka hadharani namba za simu na
majina ya maafisa usalama aliodai wako zaidi ya 22.
Amesema kuwa pia
wamenasa taarifa za maofisa hao za kumtumia Kagenzi muda wa maongezi zaidi ya
shilinigi milioni saba kwa nyakati tofauti.
Chanzo ni mwanahalisi
Online
Hakuna maoni
Chapisha Maoni