HABARI KUBWA LEO,RAIS KIKWETE KUUMBUKA,NI KURA YA MAONI,DOKTA SLAA ASEMA ANAOTA NDOTO ZA MCHANA SOMA HAPA KUJUA
UWEZEKANO wa
Watanzania kupiga kura ya Maoni ya
Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la katiba kama inavyong’ang’aniwa na
Rais Jakaya kikwete na Chama cha Mapinduzi CCM kwamba Kura hiyo ipigwe Tarehe
30 April mwaka huu,sasa umeota Mbawa,Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo
Kukwama huku kwa kura ya maoni
kunatokana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC,kushindwa katika uandikishaji
wapiga kura unaofanyika kwa mfumo wa Biometric Voters Regislation,(BVR)
kutokana na ukosefu wa Vifaa pamoja na kupewa mda mdogo.
Kwa Mujibu wa Mtoa Taarifa wetu kutoka
Kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC ameumbia Mtandao huu kwa sasa wako mbioni
kusitisha zoezi la kura ya Maoni ya kuamua Katiba pendekezwa.
“Sikufichi hapa tunafosiwa na Rais
tufanye tuwezavyo tuwe tumemaliza Mwezi wa nne wakati uwezekano ni mdogo,kwasababu
Daftari la kudumu haliwezi kukamilika kwa mda huo.yaani kama vifaa vikiwepo
vyote vinavyoitajika basi Daftari linaweza kukamilika mwishoni mwa mwezi
juni,yaani hapa hata wafanyaje hiyo kura
haipigiki mwezi wanne”ameeleza.
Kuibuka kwa taarifa hizi kunakuja siku
chache baada ya vyanzo vyetu kuambia mtandao huu kwamba Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi ccm,CC kilichoketi
mwishoni mwa wiki iliyopita kilichofanyika chini ya Rais Jakaya Kikwete Ikulu
Jijini Dar es Salaam kimekiri kwamba kura ya maoni kwa sasa haitoweza kufanyika
kama ilivyopangwa.
Baadala yake Chama hicho kwa kumtumia
Rais Jakaya Kikwete kitangaza mda wowete kutoka sasa Siku tofauti ya Kupiga
kura ya Katiba hiyo iliyopendekezwa ambayo inatokana na Katiba iliyojaa utata
wa Hali ya juu katika kupitishwa kwake ndani ya Bunge.
Taarifa za Kumanika ambazo mtandao
huu umedokezwa zinazidi sema hadi kufikia jana,NEC ilikuwa na mashine 250 tu za
kuendesha zoezi hilo,huku matatizo mengi yakiwa yamejitokeza katika
uandikishaji wake unaoendelea Mji mdogo wa Makambako Mkoani Njombe.
Mtoa taarifa huyo alizidi kuambia
mtandao huu kwamba Shehena ya Mwisho ya Vifaa inatarajiwa kuwasili nchini
katikaki ya mwezi Juni mwaka huu.
Kwa mujibu la Andishi laNEC lilisema
tume hiyo inahitaji mashine 15,000,Lakini serikali imeridhia kununuliwa mashine
8000,jambo la kushangaza NEC imepewa Mashine 250 tu kuendesha zoezi hilo ,Mradi
huo ambao unagharimu zaidi ya Bilioni 293 za kitanzania.
Kulazimishwa huko na Rais Kikwete
kwa tume ya uchaguzi ili kuharakisha
uandikishaji wa wapiga kura kunakuja huku ikiwa tayari vyama vikuu vya Upinzani
nchini kupitia umoja wao kutaka kura hiyo ya Maoni isitishwe kwa kuwa haitoweza kufanyika kwa ufanisi na
kwamba badala yake serikali iwekeze nguvu zake katika kufanikisha uchaguzi mkuu
utakofanyika baadae mwa mwaka huu.
Mbali na Vifaa vya uandikishaji huo,umekuwa
na mapungufu mengi yamejitokeza ambao watendaji wa NEC wamethibitisha kutokea.
“Waandikishaji wanababaika,watu
wengi,wanapanga foleni kutwa zima,halafu mara waambiwa kamera,halafu mara
wanaambiwa mashine mbovu tena wanaambiwa kamera imegoma”
“La ajabu
zaidi tumeshuhudia mashine imeshindwa kusoma alama za vidole wenye usugu”
ameeleza mtoa taarifa wetu wa NEC aliyoko Makambako
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa ameuoambia Mtandao huu
kwamba kwa sasa ni wazi Rais Jakaya kikwete anaota ndoto ya za Mchana mchana
kuhusu upigaji kura wa Katiba iliyopendezwa na Bunge, kwani hata wanaomzunguka wanamdanganya.
‘Kura maoni
hawezi kufanyika katika mda huu wanaosema wao,kwasasabu mpaka sahivi tume hiyo
ipo Kwenye kata tatu tu huko Makambako tu na wametumia wiki zaidi nne,je hebu kata
za nchi nzima watatumia mda gani, ambazo
zipo zaidi ya mia nne ?tunavyosema kwamba kunaubabaishaji ndio huu”amesema
Dokta Slaa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni