JIMBO LA UKONGA LAZIDI KUTEKWA NA CCM,BODABODA WAAPA KUFA NAE MBUNGE ALIYOPO,SOMA HAPA KUJUA
CHAMA Cha Mapinduzi
CCM,kinazidi kujihakikishia kushinda nafasi ya Ubunge kwenye Jimbo la Ukonga lililopo
Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kwenye uchaguzi Mkuu utakaofanyika
mwishoni mwa Mwaka huu.Anaandika KAROLI VINSENT,Endelea nayo.
Jimbo
hilo la Ukonga ambalo linaongozwa na Mbunge mwanamama Eugean Mwaiposa
,kwa sasa ni wazi dalili zinaonekana atazidi kupeta kwenye Uchaguzi huo,baada
ya Vijana Madereva maarufu Bodaboda wa Jimbo hilo kuibuka na kuaapa kumpigania
ashinde tena kwenye kiti hicho.
Kiapo hicho Kimtangazwa na Bodaboda hao
mda huu Jijini Dar Es Salaam wakati wa kufunga Semina iliyoandaliwa na Mbunge
huyo kwa ajili Bodaboda hao, yenye lengo ya kuwapa mafunzo ili kujikinga na
Ajali mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakumba.
Ambapo wakitoa kiapo hicho kwa pamoja
Bodaboda zaidi ya Mia tano kutoka Jimbo la Ukonga wamesema hawaoni sababu ya
kutomuunga mkono mwanamama huyo kwani amekuwa ni mtu pekee anayewajali wananchi
wenye lika zote hususani wao bodaboda.
Aidha, Bodaboda hao wamesema kwa sasa
watahakikisha wanawashawishi Bodaboda wengine pamoja na wananchi wa Jimbo la
Ukonga kumchagua Mbunge huyo kwa kuwa ni Kimbilio lao.
Naye Mbunge Mwenyewe Mwaiposa amewashukuru
sana bodabosa hao kwa kujua uwezo wake wa kazi na akawataka kuonyesha
ushikamano katika masuala ya Maendeleo ya Jimbo hilo kwa kipindi kifupi
kilichobakia.
Kuibuka kwa
Bodaboda hao kunampa wakati Mgumu Meya wa wa Wilaya ya Ilala Bwana Jerry Slaa
ambae inadaiwa na marafiki zake wa karibu ambao wanasema Meya huyo anainyemelea
nafasi hiyo.
Jerry Slaa
ambaye ni Diwani wa kata ya Majani ya Chai iliyopo katika Jimbo hilo na pia ni
Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha mapinduzi cc, amekuwa akiandaa mipango
inayoitwa ni ya ‘Kimyakimya”ya kumrithi mwanamama huyo mwenyeji wa Mkoa wa
Mbeya.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni