HABARI ILIYOTIKISA JIJI-PINDA AMWAGA MANYANGA,NI KUSAKA URAIS,UFISADI WAKE WAMALIZA KABISA SOMA HAPA KUJUA
MIZENGO Pinda na Bernard Membe, tayari wamejiengua katika orodha
ya wanaosaka urais kupotia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaandika
Saed Kubenea…(endelea).
Ni vigumu kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri,
Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard
Membe, kufanikiwa kupenya katika mbio zao za kusaka urais, Chanzo chetu kimeelezwa.
“Hawawezi kupitishwa na chama chao. Lakini
hata wakipita, wawili hawa hawatakuwa na nafasi ya kushinda katika sanduku la
kura la jumla,” ameeleza waziri mmoja mwandamizi serikalini.
Matukio mawili makubwa yanatajwa kuwa na
athari mbaya sana kwa Pinda na tayari yamesambaratisha moja kwa moja “mradi”
wake wa kutaka urais.
Matukio hayo, ni mahakama ya
kadhi na kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Escrow.
Kiongozi mmoja wa ngazi ya juu ndani ya
CCM amesema, “Pamoja na Pinda kuponyoka kwenye kashfa ya Escrow, lakini tayari
amejimaliza kisiasa.”
Anasema, “Pinda amejidhoofisha sana
katika sakata la Escrow kwa kuwa wananchi wanajua yule Singasinga walikutana
Ikulu kabla ya kukutana na Rais Jakaya Kikwete; na kutoka hapo ndipo alipoamuru
kukwapuliwa kwa mabilioni ya shilingi BoT.”
Pinda ni mmoja wa watuhumiwa muhimu katika
ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow.
Kwa mujibu wa andishi la Gavana wa Benki
Kuu (BoT), Prof. Benno Ndullu, makubaliano ya kugawa fedha za umma kwa
Harbinder Singh Sethi “yalipata baraka za mkuu wa nchi ambaye ni Rais Jakaya
Kikwete na waziri mkuu Pinda.”
Pinda alifahamu kuwapo makubaliano ya
kuhamisha fedha, kinga dhidi ya madai au mashitaka baada ya malipo; na kukwepa
kulipa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Anatuhumiwa kutotimiza wajibu wake;
kutojiridhisha na uhalali wa malipo na kushindwa kumshauri vema Rais Kikwete
ambaye siyo mwanasheria, juu ya utata ulioibuka kuhusu kampuni mpya ya Pan
African Power Solution (PAP), kumiliki hisa katika IPTL.
Aidha, kiongozi huyo anataja hatua ya
Pinda ya kujiingiza katika “Mahakama ya Kadhi,” imezidisha kumomonyoa mpango
wake wa kusaka urais.
“Hili la Mahakama ya Kadhi alilotwisha huyu
bwana (Pinda) haliwezi kumuacha salama. Ni lazima litamuangusha.”
Hoja ya kuanzishwa Mahakama ya
Kadhi nchini, tayari imeibua mvutano mkubwa, hasa baada ya viongozi wa
madhehebu ya Kikirsto kupinga kuanzishwa kwa mahakama hiyo.
“Sakata la Mahakama ya Kadhi” lilianzia
ndani ya Bunge Maalum la Katiba, pale Pinda alipoahidi viongozi wa madhehebu ya
Kiislamu kuwa serikali itaanzisha mahakama hiyo.
Pinda alitoa ahadi hiyo ili kuwalainisha
baadhi ya Waislamu waliokuwa wameapa kutopigia kura vifungu vya rasimu vya
katiba ikiwa suala la Mahakama ya Kadhi halitaingizwa ndani ya Katiba Mpya.
Naye Membe anatajwa kujiondoa katika
mbio hizo za urais kwa kile kinachoitwa, kijiingiza katika “kupigania OIC” na
kujiegemeza kwa Rais Jakaya Kikwete.
Membe amekuwa akiliambia Bunge, tangu
Agosti 2008, kuwa Jamhuri kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC);
ambako kunadaiwa kuwa moja ya vipengele vyake vya katiba, vinadaiwa kutaka nchi
kujiegemeza kwenye dini.
“Sakata la OIC” liliibuka kwa mara ya
kwanza nchini mwaka 1993, pale uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ) chini ya Dk. Salmin Amour, ulipoamua kujiunga na jumuiya hiyo.
Hatua ya Zanzibar kujiunga na OIC ilizua
mvutano mkubwa miongoni mwa viongozi wa juu wa serikali; jambo ambalo
lilisababisha waziri mkuu wa wakati huo, John Malecela na Katibu Mkuu wa CCM,
Horace Kolimba kufutwa kazi.
Mwingine aliyefutwa kazi katika sakala
hilo, ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Ahmed Hassan Diria.
“Huyu Membe ameshindwa kusoma
alama za nyakati. Amejimaliza katika OIC na sasa anajiegemeza kwa Kikwete kwa
lengo la kutaka kuwa rais. Hatafanikiwa,” anasema ofisa mmoja mwandamizi katika
idara ya usalama wa taifa.
Amesema, “Kila mmoja anajua
kuwa Kikwete hana ubavu wa kumpa mtu urais. Hivyo kujiegemeza naye, ni kupoteza
muda.”
Chanzo ni
Mwanahalisi Online
Hakuna maoni
Chapisha Maoni