KASHFA YA MABEHEWA 'FEKI' KUMTESA MWAKYEMBE,SASA AJIMALIZA KISIASA,SOMA HAPA KUJUA
Kuna kila dalili kwamba
uhamisho wa Waziri Dk. Harrison Mwakyembe (pichani) kutoka Wizara ya Uchukuzi kwenda
Afrika Mashariki, akibadilishana nafasi na Samuel Sitta, ni sehemu ya
kumwepusha na kadhia ya kashfa ya mabehewa feki ambayo hadi sasa imegundulika
kuwa ni kashfa nyingine inayoitafuna Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).
Uchunguzi huru
umegundua kuwa hatua ambazo zilianza kuchukuliwa na Sitta katika Mamlaka ya
Bandari Tanzania (THA), nako TRL zimeanza kutikisa baada ya kubainika kwamba
mabehewa ambayo yaliingizwa nchini kutoka China na kupokelewa na Dk. Mwakyembe
kwa mbwembwe zote kisha kubainika hayana viwango, wakubwa wa kampuni hiyo
walijua hilo, lakini wakafunika kombe kwa kuwa wakubwa walipeana zabuni kwa
njia ya kujuana.
Habari
zinasema kamati iliyoundwa na Sitta kuchunguza kashfa ya uingizaji mabehewa
hayo kutoka India, tayari imeibua mambo mazito ambayo yanaongeza orodha ya
kashfa za ulaji na ufujaji wa fedha za umma uliosimamiwa na baadhi ya viongozi
wa serikali wakitumia madaraka yao vibaya.
Kwa mujibu wa
vyanzo vya habari kutoka TRL, uingizaji wa mabehewa hayo ulifanywa na Kampuni
ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ya India kwa kushirikiana
na mfanyabiashara mmoja nchini ambaye kwa miaka mingi amehusika katika kadhia
nyingi za kujipatia fedha kwa mikataba laghai dhidi ya serikali na mashirika
yake.
Vyanzo
vyetu ndani ya TRL vinasema kuwa kamati iliyoundwa kuchunguza kashfa hiyo ya
ufisadi wa mabilioni ya fedha, inatarajia kukamilisha taarifa yake ya uchunguzi
hivi karibuni na kuikabidhi kwa Waziri Sitta, lakini tayari imegundua madudu
mengi ikiwamo wakubwa kupokea mabehewa yenye hitilafu wakati wakijua.
Waziri Sitta
amesema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumzia jambo lolote hadi atakapokabidhiwa
ripoti ya uchunguzi.
“Suala la mabehewa
feki nimelikuta na kuna tume (kamati) iliundwa kuchunguza na inatarajia
kukamilisha ripoti yake hivi karibini, nadhani kwa sasa tungevuta subira ila
niwahakikishie wananchi sitaogopa kuchukua hatua bila kujali kashfa hiyo
inamhusu mtu au kiongozi wa namna gani,” alisema. Kashfa ya uingizaji wa mabewa
feki iligundulika mwishoni mwa mwaka jana, ikidaiwa kuwa kuna ufisadi mkubwa
umefanyika ndani ya TRL katika utoaji wa zabuni ya ununuzi wa mabehewa mapya.
Baadhi ya
mafundi wa TRL wanasema kuwa mabehewa hayo ni mabovu na hayaendani na vipimo
vya reli ya kati.
Udhaifu wa
mabehewa hayo uligundulika baada ya kufanyiwa majaribio, kufuatia mengi ya yale
mapya 25 aliyopokea Dk. Mwakyembe kupata ajali katika mazingira ya kutatanisha,
huku ikidaiwa kuwa hayana ‘stability’ yakiwa juu ya reli.
“Unajua hata
yale ya mizigo mengi yalianguka sana. Sasa ikaonekana hebu na haya ya abiria
yachekiwe vizuri, nakuambia matokeo yake ni balaa kama yangeachwa kusafirisha
abiria. Ingekuwa ni kilio nchi nzima,” alisema mtaalam mmoja wa masuala ya reli
kwa sharti la kutokutajwa jina Mtandaoni.
Mabehewa hayo tangu yapokelewe takribani
miezi tisa sasa, hayajawahi kusafirisha abiria.
Mtaalam huyo
aliongeza kuwa kilichofanyika ni uongozi wa TRL wakishirikiana na wakubwa
wizarani kuengua jopo la mafundi wa TRL na kuingiza mabehewa hayo kwa kuwa
tayari wakubwa walikuwa na mtu wao katika tenda hiyo.
Dk. Mwakyembe
alizindua mabehewa mapya 25 ya kubebea kokoto aina ya ‘Ballist Hopper Bogie’
(BHB), kutoka kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited
yenye thamani ya Sh. bilioni 4.316 kwa ajili ya uimarishaji wa Reli ya Kati.
Upokeaji wa
mabehewa ya mizigo ulifuatiwa na tukio jingi la kushuhudia upokeaji wa mabehewa
mengine ya abiria Julai 24, mwaka jana Dk. Mwakyembe akiwa mmoja wa
mashuhuda.
Alipoulizwa na Chanzo Changu kwa njia ya simu jana kuhusiana na kashfa ya
mabehewa feki TRL, Mwakyembe alisema: "Hivi sasa niko nje ya nchi...
vyombo vya habari vimesharipoti sana suala hili. Watu tayari walishachukuliwa
hatua, inawezekana wewe (mwandishi) hujui, wenzako wameandika sana kuhusu suala
hili, na watu walishachukuliwa hatua."
Katika hafla ya
upokeaji na ushushaji wa mabehewa hayo katika Bandari ya Dar es Salaam, Dk.
Mwakyembe alisema ununuzi wake ni sehemu ya utekelezaji wa makakati wa ‘Matokeo
Makubwa Sasa’ (BRN), ambao umelenga kuhakikisha usafirishaji wa reli unaimarika
kwa ajili ya kuhimili usafirishaji wa abiria na mizigo, hivyo kusaidia utunzaji
wa barabara za lami zinazojengwa kila kona nchini kwa sasa.
Vyanzo vya habari
kutoka TRL vinasema kuwa uhamisho wa Dk. Mwakyembe kutoka Uchukuzi, ni mkakati
wa kumwepusha na kadhia yoyote ambayo inaweza kulipuka wakati wowote kutokana
na zabuni hiyo ambayo inaonekana kama aina nyingine wa wizi wa wazi.
Mbali na Dk.
Mwakyembe, menejimenti ya TRL nayo iko kikaangoni tangu Sitta aunde kamati ya
kuchunguza kashfa hiyo.
CHANZO: NIPASHE
Hakuna maoni
Chapisha Maoni