HABARI KUBWA LEO-KAFULILA AMBAMIZA KIKWETE,NI KUHUSU UFISADI WA ESCROW,AIPINGA KAFALA YA TIBAIJUKA SOMA HAPA KUJUA
MBUNGE wa
Kigoma Kusini David Kafulila (pichani) ameendelea kuindama Serikali ya Rais Jakaya Kikwete
kuhusu Sakata ukwapuaji wa Mabilioni ya Shilingi kwenye Akaunt ya Tegeta Escrow-
Baada ya hivi sasa kuivaa tena serikali na
kutaka iache ubabaishaji kwenye sakata hilo na kuilazimishe iwataje kwa majina ya Vigogo wa Ikulu walionufaika pesa kupitia Akaunt ya banki
ya Stanbiki.Anaandika KAROLI VINSENT Endelea Nayo hapo
Kauli ya Mbunge kafulila inakuja ikiwa
bado nchi wahisani wakiwa wamegoma kutoa
misaada kwa Serikali ya Tanzania wakitaka utekelezwaji wa Maazimio ya Bunge
kwenye Sakata la ukwapuaji mabilioni ya Escrow.
Nchi hizo wa hisani waliogoma ikiwemo
Marekani kupitia Shirika la Millenium Challenge Corporation (MCC) ambao
wamesitisha zaidi ya Sh.800 bilioni kwa awamu ya pili hadi mpaka kutekeleza
maazimio ya Bunge kuhusu sakata hilo.
Mbunge Kafulila alitoa kauli hiyo leo
wakati alipokuwa anazungumza na Kituo cha Redio cha Magic Fm katika kipindi cha
Morning Magic ambapo amesema kwa sasa kitendo cha Serikali kuwashtaki watu
waliopewa pesa kupitia banki ya Mkombozi na kuwaacha waliochukua pesa kupitia
akaunt ya Stanbiki ambao anadai wako vigogo wa Ikulu pamoja na Mawaziri ni kuwadanganya watanzania na kuficha ukweli.
“tumepata taarifa kwamba waliochukua
pesa kupitia banki ya Stanbiki wapo vigogo wa ikulu lakini leo serikali
inaficha Suala hili na kuweka wazi majina ya watu waliochukua pesa kwenye banki
ya mkombozi ,hata hivyo hii inaweka imani mbovu kwa serikali”amesema Kafulima.
Kafulila ambaye ni mtu aliyeliibua Sakata la Ufsadi wa
Escrow Bungeni mwaka jana, ameongeza kuwa kama kungekuwa na serikali makini
ingechukua hatua kali kwa viongozi
walioruhusu pesa kutoka pale Benk kuu (BOT) wakiachiwa.
“Huyo Werema amehusika kwa kiasi kikubwa
kuruhusu pesa kutoka ,muongo kama waziri leo ameishia kujiuzulu wakati jina lake limehusika
katika kutoka pesa lakini awachukuliwi hatua na tena hapa tunapata mashaka
makubwa sana na hata kuhusika kwa ikulu kuchukua pesa kwenye Akaunt ya Stanbik
hii inaoshesha wazi hakuna kinachotekelezwa”Ameongeza Kafulila.
Kuhusu nchi
wahisani kugoma kutoa misaada kuhusu sakata hilo
Mbunge Kafulila amesema nchi za
wahisani wanajua sakata zima la escrow kuriko watanzania wenyewe,huko akisema Rais Kikwete haeleweki anavyowachukulia hatua
watu waliopewa pesa kupitia benki ya Mkombozi.
“Leo anavyowachukulia hatua watu
waliopewa pesa na Rugimalira hata ujawakamata na hata Seth huyo singasinga
hawachukuliwi hatua wala kupelekwa mahakamani,na mpaka leo huyo singasinga yupo
tena bado anaendeleaa kumiliki mitambo hiyo huku TANESCO bado wakilimpa billion tatu kwa mwezi,ndio maana
nchi za marekani wanaona wazi hii,kwamba serikali haipo makini na tutakosa misaada
tu’amesema Kafulila.
Alipouulizwa
anazungumziaji kauli wanazotoa Viongozi waliopandishwa kwenye Baraza la Maadili
ikiwemo kauli aliyoitoo Profesa Anne Tibaijuka kuwa Milioni kumi ni hela ya mboga.ambapo kafulila amesema hizo
ni kauli zinazoonyesha kwamba kuna ufisadi mkubwa hapa nchini.
“Kwamba watu
wanaona ufisadi huu mkubwa wanashtuka,lakini wahusika wenyewe wa Ufsadi wanaona
ufisadi wa kawaida ,kwani wanajua kunaufisadi mkubwa kuriko huu wa escrow ndio
maana wanasema hivyo”
Hakuna maoni
Chapisha Maoni