MFUMUKO WA BEI UMEONGEZA,SHILINGI YA TANZANIA YAZIDI ANGUKA,TAKWIMU YATAJA SABABU,SOMA HAPA KUJUA
OFISI ya
Taifa ya Takwimu imesema Mfumuko wa bei
ykwa mwezi ulioisha wa pili umeongezeka
hadi asilimia 4.2 kutoka asilimia 4.0 ilivyokuwa mwezi January mwaka huu,Anaandika
KAROLI VINSENT Endelea nayo.
Akitangaza Hali hiyo Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na
Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa
Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amesema
Mfumuko huo wa Bei umeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa
mwaka ulioshia
Aidha, Bwana Kwesigapo amesema kuongezeka
mwa mfumuko wa bei wa mwezi Februari mwaka huu kumechangiwa na kuongezeka kwa
bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Februari.
Alibainisha kuwa Mwenendo wa bei za baadhi
ya Bidhaa za Vyakula zilizoonyesha kuongezeka mwezi Februari ni pamoja na bei za Mchele asilimia (18.5)
unga wa muhogo (asilimia 9.3)nyama (asilimia 9.3),samaki asilimia 12.4 na
maharagwe asilimia 7.1.
Kwa upande Mwingine Bwana Kwesigapo
Amesema Mwenendo wa Bei za bidhaa zisizo za Vyakula zilionyesha kuongezeka kwa
mwezi Februari ikilinganishwa na mwezi huo huo kwa mwaka jana ni pamoja na
mavazi ya Wanaume ambayo yameongezeka kwa Asilimia 4.7.mavazi ya wanawake
asilimia 3.3,mkaa asilimia 5.1 mashuka
asilimia 3.1 pamoja na gharama za kumuona Daktari kwa asilimia 11.2.
Kuhusu Thamani ya Shilingi ya
Tanzania
Bwana
kwesigapo amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na
huduma umefikia shilingi 64 na senti 59 mwezi februari ikilinganishwa na
Shilingi 65 na senti 60 ilivyokuwa mwezi januari
Hakuna maoni
Chapisha Maoni