TMA YAPINGA KUPOTEZA BILIONI 1.2 KWENYE KODI,SOMA HAPA KUJUA
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dokta Agnes Kijazi akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaa |
MAMLAKA ya
Hali ya Hewa nchini(TMA) imekanusha taarifa zilizoandikwa na Vyombo mbalimbali
vya Habari ambazo zilikuwa zinasema kwamba Mamlaka hiyo inapata Hasara ya bilioni
1.2 kwa mwaka kutokana na wao kupanga kwenye Jengo la Ubungo Plaza Jijini Dar
es Salaam.Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo
Akikanusha Taarifa hizo Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Hali ya hewa nchini (TMA)Dokta Agnes Kijazi leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari ambapo amesema taarifa hizo sio za kweli zinalengo la
kupotosha umma kwani ukweli uliopo ni kwamba Mamlaka hiyo imepanga kwenye
ghorofa la tatu na la nne kwenye jengo la Ubungo Plaza na akabanisha wanatozwa kodi ya milioni 132,kwa miezi mitatu
ambapo kwa mwaka mamlaka hiyo inalipa
Milioni 528 sio Bilioni 1.2 .
Aidha,Dokta Kijazi amesema kwa sasa
Mamlaka hiyo iko mbioni kujenga jengo lao wenyewe ambapo tayali wameshapata
kiwanja kilichopo Ubungo Jijini hapa na kwa sasa wako katika harakati ya
kutafuta pesa kwa ajili ya kufanya ujenzi,na ameongeza kuwa pindi ujenzi
ukikamilika itawasaidia katika kufanya kazi kwa uhuru kuriko sasa.
Katika hatua Nyingine Mamlaka hiyo
imetoa taarifa kuhusu Mvua za barafu zilizonyesha wiki iliyopita mkoani Kahama
na kupelekea vifo vya watu 41 na kutokea
madhara ya kuharibika vitu mbalimbali ,ambapo amesema hali hiyo ya Mvua
ni tukio geni hapa nchini na kusema inatokana na misiguano ambayo ipo katika
wingu angani.
Dokta kijazi akawataka wananchi
wasipuuze taarifa zinazotolewa na Mamlaka hiyo,kwani taarifa wanazotoa zina
ukweli na zitawasaidia wananchi kujikinga na majanga ambayo yanaweza kutokea
kutokana na Mvua kali zinonyesha mara kwa mara.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni