KATIBA YA SITTA PASUA KICHWA,WANAHARAKATI WAAPA KUFA NA KIKWETE MAHAKAMANI SOMA HAPA KUJUA
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia) akikabidhi nakala ya Katiba Inayopendekezwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya |
KITUO cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), kinatarajia kuiburuza Serikali mahakamani kwa kile
kinachodaiwa ni “kuharibu mchakato wa katiba mpya”. Anaandika Pendo
Omary…(endelea).
Kauli hiyo imetolewa na Hussein
Sengu- Afisa Sheria dawati la uangalizi wa serikali, wakati wa ugawaji wa
Katiba inayopendekezwa kwa Asasi za Kiraia, taasisi za dini, vyama vya kihiyari
na taasisi za serikali.
Ugawaji huo umefanywa leo na Dk.
Asha-Rose Migiro-Waziri wa Katiba na Sheria katika viwanja vya Karimjee jijini
Dar es Salaam.
Sengu ambaye aliwakilisha LHRC
katika hafla hiyo, amesema, “tangu mwanzo msiamo wa Kituo chetu unapinga
mchakato huu. Tayari mchakato mzima wa Katiba Mpya ni batili, Haukuwa
shirikishi. Umetekwa na serikali.”
“Baada ya shughuli hii leo,
tunaendelea na kampeni ya kupinga Katiba inayopendekezwa. Tukianza rasmi kwa
kuishitaki serikali mahakamani muda wowote kuanzia sasa. Tutafungua Kesi ya
kikatiba,” amesema Sengu.
Kwa mujibu wa Sengu, baadhi ya
vitendo vinavyofanywa na watumishi wa serikali akiwemo Rais Jakaya Kikwete na
waziri Asha-Rose Migiro kuipigia chapuo ya ‘ndiyo’ Katiba pendekezwa ni kinyume
na matakwa ya kisheria yanayoitaka serikali kutokuwa na upande katika mchakato
huo.
Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Jumuia
ya Mabohora nchini, Zainaddin Adanjee amesema “Sisi tumeipokea Katiba
inayopendekezwa, tutaisambaza. Msimamo wetu ni kila mtu kwa hiayari yake afanye
maamuzi. Asilazimishwe kukubali kitu ambacho hakitaki”.
Naye Dk. Migiro amesema hatua hiyo
ni ya pili ambapo tayari hatua ya kwanza ilikuwa ya kugawa nakala milioni mbili
za Katiba hiyo nchi nzima.
“Tayari nakala milioni mbili
zimesambazwa mikoa yote. Kila kata tumepeleka nakala 300. Zanzibar tumepeleka
nakala 200,000. Nakala 658,700 zitagawiwa kwa wizara na taasisi za serikali,
taasisi za dini, asasi za kiraia na vyama huru,” amesema Migiro.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni