HABARI KUBWA LEO CHENGE KUIBURUZA CCM MAHAKAMANI,KUPINGA KUFUKUZWA KWAKE CCM,SOMA HAPA KUJUA
MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (pichani), yuko njiani
kukifikisha mahakamani Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Saed Kubenea…
(endelea).
Anapinga kusimamishwa ujumbe wa mkutano
wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC) wa chama hicho.
Nape
Nnauye, Katibu wa Itikadi na uenezi, alitangaza mwishoni mwa wiki kuwa Chenge
na wenzake wawili – Prof. Anna Tibaijuka na William Ngeleja – wamesimamishwa
uongozi ndani ya chama hicho.
Prof. Tibaijuka ambaye ni mbunge wa
Muleba Kusini, amesimashwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC). Naye Ngeleja
aliyeshikilia ubunge katika jimbo la Sengerema, ni mjumbe wa NEC.
Alisema, viongozi hao watatu
wamesimamishwa uongozi kwa makosa ya maadili; hatima ya uongozi wao utajulikana
baada ya vikao vya maadili kumaliza kazi zake.
Chenge hakupatikana kufafanua madai hayo
kwa kutwa nzima ya jana-simu yake kili ilipopigwa, ilijibiwa kuwa “ahasante kwa
kutumia mtandao wa Vodacom, huduma kwa mteja unayempigia zimezuiwa kwa
muda-jaribu tena baadaye”.
Mtoa taarifa anasema, Chenge ameamua
kwenda mahakamani baada ya kujiridhisha kuvunjwa kwa taratibu katika kufikia
maamuzi hayo. Hakuzitaja taratibu hizo.
Amesisitiza, “Ni lazima Chenge
atakwenda mahakamani kuomba amri ya kuzuia uamuzi huu wa CCM. Kesi hii,
itafunguliwa mara baada ya kukabidhiwa barua inayomjulisha kuhusu uamuzi huo.”
Chenge,
Prof. Tibaijuka na Ngeleja, wanatuhumiwa kujipatia “mgawo” wa mabilioni ya
shilingi, kutoka kwa James Rugemalira, mmoja wa wanahisa katika kampuni ya
kufua umeme ya IPTL.
Rugemalira alikuwa akimiliki asilimia
30 ya hisa katika kampuni hiyo, kupitia kampuni yake ya VIP Engineering and
Marketing ya jijini Dar es Salaam.
Chanzo ni
Gazeti La Mwanahalisi.online
Hakuna maoni
Chapisha Maoni