MKE WA KIKWETE MATATANI,AGEUZA ASASI YAKE KUWA MTAJI WA CCM,SOMA HAPA KUJUA
RAFU mbaya za Kisiasa zilizofanywa na Chama cha Mapinduzi CCM
ndani ya Asasi inayohusu Masuala ya Maendeleo na kuwajengea uwezo( WAMA),Zazidi
kuiweka Asasi hiyo Njia panda,Mtandao huu imedokezwa.anaripoti KAROLI VINSENT
Endelea nayo
Asasi hii ambayo
ilianzishwa mara tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuingia Madarakani mwaka
2005 na kupewa jina la wanawake na Maendeleo WAMA,na kutambulishwa kupitia jina
la mke wa Rais Kikwete,Mama Salma Kikwete.
Uchunguzi uliofanywa na Mtandao huu umebaini
asasi hiyo imegeuka ya Wake wa Vigogo kutoka Ndani chama cha Mapinduzi,CCM na
kugeuka kuwa miongoni mwa asasi inayofanya kazi ya kuwaingiza madarakani
Vigogo mbalimbali wa CCM,huku ikiwa kinyume na Matarajio ya wengi kwenye Asasi
hiyo.
Kwa
mujibu wa sheria inayosimamia Asasi zisizo za Kiserikali nchini zinazuiliwa kwa
Asasi kujiingiza katika masuala ya Kisiasa,lakini kwa asasi hii ya
WAMA,inaonekana wazi kwenda kinyume kutokana kufanya kampeni ya Mgombea wa
Urais mwaka 2010 kupitia CCM.
Asasi
hii imekuwa ikipigiwa kelele na Wabunge kutoka vyama upinzani nchini kwa
kuishutumu kugeuka kuwa asasi ya chama cha Mapinduzi CCM.
Kwa mujibu wa Vyanzo vya kuaminika ambavyo
mwandishi wa Mtandao huu ameziona, zinaonyesha Jinsi Rafu ilivyofanyika katika
Asasi hiyo kutokana Wajumbe wa Juu kwenye umoja huo wa Wanawake nchini,ambao ni
Wake wa Viongozi na Makada kutoka CCM.
Chanzo hicho kilionyesha kuwa, Mwenyekiti
wa Asasi hiyo ni mke wa Rais Kikwete,mama Salma Kikwete,ambaye ni mjumbe wa
Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM (NEC-CC)kutoka mkoa wa Lindi,
Chanzo hicho pia kilimtaja Mjumbe
wa Pili ambae ni Zakhia Meghji,huyu ambae ni mweka hazina Mkuu wa CCM na Mjumbe
wa Kamati kuu cha hicho tawala ambacho ni chama pekee kikongwe ambacho kipo
madalakani kusini mwa Jangwa la Sahala.
Vilevile
Meghji,amepewa ulaji mwengine na Serikali yake ya CCM na kwa kuchaguliwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumbe la Taifa NHC.
Mjumbe mwengine wa Tatu,Mwanamwema
Shein,mke wa Dk Ali Muhamedi Shein ambaye ni Rais wa Zanzibar na Makamo
Mwenyekiti wa CCM
Chanzo hicho kilizidi kutaja hujuma pamoja na Rafu inayofanywa na chama
cha Mapinduzi kwenye Asasi hiyo kwa kumtaja Mjumbe wa Nne,ambaye Sophia Simba.Huyu
ni Mwenyekiti wa Ummoja wa Wanawake wa CCM (UWT-CCM) .
Sophia Simba,ambaye ni
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,wanawake na Watoto.ambapo kisheria anapaswa
kusimamia asasi zifuate maadili lakini ameshindwa kabisa kuisiamia Asasi ya
Wama ambayo imekuwa ikijiingiza kisiasa.
Mjumbe mwengine ni Regina
Lowassa,mke wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu mwaka 2007 kwa shinikizo la Bunge
kufuatia kuhusika na ufisadi na Kashfa ya Mkataba wa Richmoond.
Mume wa Regina vilevile ni
Mbunge wa Munduli,ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge la
Tanzania,mbaye ni pia ni miongoni mwa watu wanaotumia kila aina ya njia
kuhakikisha anakuwa Rais 2015.
Rafu hii ilizidi
kujidhilisha baada ya kubainika Mjumbe mwengine ambaye ni Blandina Nyoni kuwepo
kwenye Bodi ya Wama.mama huyu aliwai kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ambapo
alisimamishwa kutokana kuzidisha ukilitimba ofisini.
Duru zinasema Asasi hiyo,ambao
iliazishwa kuwatetea wanawake kwa kuwaondoa kwenye lindi la Umasikini kwa
kutoangalia upande wowote wa chama, lakini kwa sasa imeguka kuwa ni Asasi ya
kuwaingiza wajumbe hao pamoja na wanaume zao kubaki Kula neema ya nchi kuliko
kuwatetea wanawake.
Kwa upande wake
Mchambuzi wa Kisiasa na Msomi pia wa Masuala ya kisiasa kutoka chuo Kikuu cha
Dodoma Seiph Yahaya alisema Hakuna Jipya kwenye asasi hiyo,na ipo kwa manufaa
ya Tabaka Tawala tu.
“Sikiliza nikwambie,hapo hakuna kitu, tu hapo ni mpango wa
kuhakisha wake waViongozi wanazidi kuneimeka tu,kwani kama Asasi hiyo ingekuwa
inania Nzuri kwanini hakuna hata mjumbe yeyote kwenye bodi hiyo kutoka Chadema
wala Cuf”
“Huu ni mwendelezo wa kutudanganya watanzania kwasabu washatujua
sisi mazezeta sana,na hata mimi namshangaa sana waziri Sophia Simba na
kushindwa hata kutetea sakata hili”alisema Seiph
Hakuna maoni
Chapisha Maoni