TGNP YAZIDI KUWATETEA WANAWAKE,YAAZIMISHA SIKU YAO KWA KUTOA WITO MZITO,SOMA HAPO
Pichani Ni Mkurugenzi wa TGP Lilian Liundi akizungumza na Waandishi na Habari |
WITO
umetolewa kwa Jamii kupinga vitendo vya Ukatili kwa wanawake nchini,ambavyo
vimekuwa vikisababisha kuwepo kwa Watoto wa Mitaani.Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijinsia nchini TGNP Be Lilian
Liundi wakati kuazimisha siku ya Wanawake Duniani ambayo iliazimishwa na TGP
Ofisini Kwao ,ambapo Be Liundi amesema Lengo la maazisho hayo ni kutambua mchango
wa Mkubwa anofanya Mwanamke kiuchumi na
Kimaendeleo hapa nchini.
Aidha,amesema kuwa maadhimisho hayo
yanatoa nafasi kwa mwanamke kutambua matukio mbalimbali yanayotokea ikiwemo
kunyimwa haki zao za msingi kama vile kutogombea nafasi mbalimbali za uongozi
Jambo ambalo limekuwa likisababisha wao kushindwa kupata nafasi hizo huku
wakiwa na uwezo wa kufanya kazi hizo,
Kwa Upande wake Mtetezi na Mwanahalakati
Maarufu wa Wanawake nchini ambaye aliwai kuwa Mbunge na Waziri wa Elimu nchni
Mama Thabitha Siwale amesema Bado Jamii imeshindwa kutambua mchango wa mwanamke
huku ikizingia imepita miaka 20 baaa ya mkutano wa Bejing uliofanyika nchini
China ambao umewapa nafasi wanawake lakini bado mfume dume unazidi
kuwakandamiza.
Washiriki mbalimbali waliojitokeza kwenye siku ya Wanawake Duniani |
Alibainisha kuwa Viongozi wanawake
walioko katika Sekta za Maamuzi ya Sheria wanawajibu wa Kumtetea Mwanamke kwa
kuziondoa sheria kandamizi kama yeye alivyokuwa Mbunge alivyofanikiwa kuondo
kipengele cha Sheria kinachomyima Mwanamke kumiliki Ardhi.
Vilevile Mama Siwale aliwataka wanawake
kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali kwenye uongozi Katika chaguzi mbalimbali Mwaka huu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Octoba.
Maadhisho
hayo ya Wanawake kwa Mwaka huu yana kauli mbiu inayosema Uwezeshaji
Wanawake,Tekeleza Wakati ni Siasa
Hakuna maoni
Chapisha Maoni