Zinazobamba

JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUKUTANA NA WABUNGE LAMADA HOTEL,WAOMBA WADAU KUJITOKEZA KWA WINGI


Ungozi wa jumuiya ya Wafanyabiashara wa soko la Kariakoo jijini Dar es salaam, unawatangazia wadau wote wafanyabiashara wa soko hilo kujitokeza kwa wingi katika hotel ya Lamada iliyopo Ilala ili kujadili maswala mbalimbali wakiwa pamoja na Wabunge wote wa jijini Dar


Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Philimini Romano Chande wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa uliofanyika mapema hii leo
Amesema kuwa katika mkutano huo wanatarajia kuzungumza mengi na wabunge lakini kubwa nikujadili jinsi ya masuala ya Kodi, kwani maranyingi  wafanyabiashara wamekuwa wakipakaziwa kuwa si walipaji wa kodi huku ukweli ukiwa ni kwamba Wafanyabiashara walipaji wazuri wa kodi ya nchi
Aidha Philimini ameongeza kusema katika mkutano huo watangazungumzia masuala  mbalimbali ikiwamo suala la eneo la kufanyia biashara ni udogo wa eneo kutokana na wingi wa wafanyabiashara wanaitaka serikali iwatafutie eneo zuri na kutatua tatizo la mashine za risiti za Mamlaka ya mapato TRA ili wafanyabiashara waweze kulipa kodi ambapo kwa sasa wengi wao wamegoma kulipa, kitendo alichodai kinairudisha nyuma nchi ya Tanzania.
Kwa upande wake Katibu mpya wa Jumuiya hiyo Abdallah Ismail Mwinyi, akizungumza na mtandao huu amesema mkutano huo ni muhimu sana kwa kutatua matatizo yao yanayowahusu

Hakuna maoni