WAZIRI NYALANDU ATANGAZA KIAMA NA MAJANGILI,SASA KUTUMIA WANAJESHI KUTOKA UJERUMANI,SOMA HAPA KUJUA
WAZIRI wa
Maliasili na Utalii (pichani) Waziri Lazaro Nyalandu amewatangazia Majangili wa wanyama
wa tembo popote walipo kuachana na kazi hiyo, kutokana na Mikakati mizito
aliyoipanga ikiwemo ya Ulinzi ambao atashirikiana na wanajeshi kutoka nchini
Ujerumani,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Waziri Nyalandu ametangaza kiama hicho leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambao ulikuwa na
lengo la kuzungumzia siku ya wanyama pori duniani,ambapo amesema kwa sasa haoni
sababu ya kuendelea kuwaachia majangili kuua wanyama wetu husani Tembo.
“Kwa sasa nawapa salamu majangili
popote walipo nchini,kwamba tumejipanga nawahakikishia ni kwamba watafute kazi
ya kufanya,tumejipanga,maana hautuwezi tukawaachia watu wachache wamalize
wanyama wetu ambao ni hazina kubwa sana nchini na duniani”amesema Waziri
Nyalandu.
Waziri Nyalandu ameongeza kuwa kwa sasa
wameamua kushirikiana na Wanajeshi kutoka nchi za ulaya kuja kuwafundisha ujuzi
Askari wa wanyama pori, ujuzi wa kivita ili waweze kupambana na Majangili.
Alibainisha kuwa haona haja ya
watanzania kuwavumilia watu wa aina ya majangili ambao wanataka kuharibu neema
ya kipekee ya nchi yetu.
“Leo Tanzania ni nchi ya pili kuwa na
wanyama pori wengi sana ukitoa nchi ya Brazili,na pia Tanzania ni nchi ya pili
barani Afrika kuwa na tembo wengi
sana,sasa neema hii yote hii tuwaachia majangili waifute nasema haitowezekana
na lazima tuwamalize”Amebainisha Waziri
Nyalandu.
Aidha, Waziri Nyalandu amewataka
watanzania kushirikiana na Askari wa wanyama pori kupambana na Majangili popote
walipo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni