HABARI ILIYOTIKISA JIJI-KIKWETE AIVULIA KOFIA AZAM MEDIA,SOMA HAPA KUJUA
RAIS Jakaya
Kikwete leo ameshindwa kujiuzuia baada ya kutoa mshangao wake baada ya kuona
ubora wa Studio za kisasa za kurushia Matangazo
ya Kituo cha Azam TV ambazo zinalingana na Runinga Bora Duniani
kama vile CCN,BBC,Al-Jazeera,DW,Anaandika
KAROLI VINSENT Endelea nayo
Azam tv ambayo inamilikiwa na Mfanyabiashara
Maarufu Nchini Said Salim
Bakhresa wamejenga Studio hizo ambazo zipo Tabata Relini Jijini Dar es
salaam zenye Thamani ya pesa za kitanzania Zaidi ya bilioni 56.
Akizindua Studio hizo Bora za kisasa
Kabisa kuwepo Kusini mwa Jangwa La Sahala Mda huu Jijini Hapa, Rais Jakaya
Kikwete Amemwagia sifa Mfanyabiashara huyo na kusema ameleta mapinduzi makubwa katika sekta ya Habari
nchini na kuwataka wamiliki wengine wa Runinga nchini kuiga mfano na
Mfanyabiashara huyo.
Kuzinduliwa huko kwa Studiao hizo za
kisasa,kunakuja ikiwa Kampuni hiyo ya Azam tayari imeshapata Leseni ya kurusha
Moja kwa Moja mechi ya Ligi kuu ya Vodacom ya Tanzania Bara,na pia wako mbioni
kuonyesha pia Ligi kuu mbalimbaliza Soka Afrika Mashariki na sasa ameshapiga
hodi nchini Uganda.
Mbali na Runinga Mfanyabiashara huyo pia
ameanzisha Radio yake hapa jijini.
Wafanyakazi wanena.
Wafanyakazi mbalimbali wa
Runinga ya Azam waliozungumza na mwandishi wa Mtandao huu kwa Sharti ya
kutotaja majina yao mtandaoni, wamemwagia sifa Mfanyabiashara huyo na kusema ni
Mmiliki pekee nchini, wa Vyombo vya Habari anayelipa vizuri.
‘Sikifuchi mimi nimefanya kazi kwenye
Vyombo mbalimbali nchini kusema kweli kwa sasa nilivyohamia hapa Azam Media
huyu mmiliki wetu anatujali sana kwanzia vitendea kazi na pia malipo mazuri”
Wimbi la watangazaji
nchini kuhamia Azam media.
Taarifa za Kuaminika
ambazo mtandao huu umezipata unasema kwa sasa Mfanyabiashara huyo ameweka
mipango ya ,kuwachukua watangazaji mbalimbali kutoka Redio na televisheni kuja
kuhamia kwenye Redio yake mpya.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni