BODABODA WAZIDI LILIWA,NI KUHUSU BIMA YA AFYA,MBUNGE MWAIPOSA ASEMA YAKE SOMA HAPA KUJUA
WITO
umetolewa kwa Waandesha pikipiki Maarufu “Bodaboda”Kujiunga na Huduma za Bima ya Afya
ili iwasaidie pindi wanapopata Ajali ambazo zimekuwa zikiongozeka kila Kukicha.Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo hapo
Wito huo umetolewa mda huu Jijini Dar es
Salaam na Afisa mtekelezaji wa Mfuko wa Bima ya Afya Bwana Goefrey Tumain
wakati ya Semina ya siku moja kwa Madereva
bodaboda walioko Jimbo la Ukonga Jijini hapa ambapo Bwana Tumain amesema
Bodaboda wengi wamekuwa wakitesaka sana pindi wapatapo ajali huku wakisota kwa
kukosa matibabu kwasababu hawako kwenye huduma ya Bima ya Afya.
Bwana Tumain ameongeza kuwa kwa sasa Mifuko
ya Bima ya Afya imewapa nafasi bodaboda ambao watajiunga kwenye vikundi vyao
kwa kutoa pungufu ya kulipia Gharama ya Elfu 76800 kwa mwaka.
Amebainisha kuwa Bodaboda ambao hawapo kwenye Vikundi watatozwa
Gharama ya tofauti ambayo ni Laki tisa kwa mwaka.
Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la
Ukonga Eugin Mwaipopo amewaomba Bodaboda kutii sheria zilizowekwa na Mamlaka
husika na ameitaka Serikali kuangalia
upya zuio waliloweka kwa Bodboda kutoingia katikati jiji kwa kusema kwamba
kunawarudisha nyuma kwenye maendeleo bodaboda hao kwakukosa pesa.
Vilevile Mbunge huyo amesema kitendo
cha kuwazuia kwenda mjini kutasababisha kuongezeke kwa vitendo vya wizi kwenye
maeneo mbalimbali huko ikifamika kwamba madereva hao wa Bodaboda wamekopa pesa
kupitia sehemu mbalimbali.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni