Zinazobamba

HABARI KUBWA-KAMBI YA LOWASSA YABOMOKA,NI ILE YA KANDA YA ZIWA,KAFALA PROF-TIBAIJUKA YAIBUA MAPYA,SOMA HAPA KUJUA


Kambi ya Waziri Mkuu wa Zamani , Edward Lowassa (pichani) inayoaminika kuwa ni ya siku nyingi zaidi katika kinyang'anyiro cha kusaka uteuzi wa kugombea urais kupitia CCM , hatimaye imeanza kusambaratika baada ya mmoja kati ya vigogo wake wa kutegemewa kwa mikoa ya Kanda ya ziwa kuanza kuisaliti kimya kimya,Anaandika KAROLI VINSENT,Endelea nayo
       Chanzo hicho cha habari cha kuaminika kutoka kambi hiyo kigogo huyo ambaye alichangia kwa sehemu kubwa kujenga ngome imara ya LOWASSA katika Kanda ya Ziwa, hivi sasa amegeuka kimyakimya huku ikielezwa kuwa anayeibomoa ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli.
          Inasemekana kigogo huyo ambaye pia ni mjumbe wa NEC na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM amekwenda kumshawishi Magufuli kwamba achukue fomu ya kugombea nafasi hiyo ya urais.
          Lowassa ni miongoni mwa Makada kutoka chama cha Mapinduzi CCM wanaosaka Urais kwa udi na Uvumba mwaka huu,huku ikionekana anauswahiba mbaya na Rais Jakaya Kikwete ambaye lowassa alitumia pesa zake mwenyewe kumingiza madarakani mwaka 2005.
        Habari zaidi zinasema kuwa Wajumbe wengi hasa wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM hawana imani tena na LOWASSA kutokana na sababu mbalimbali . Wajumbe hao wamesema sasa hawataangalia nani ana nguvu kiasi gani ila watazingatia zaidi matakwa ya chama kwamba kinamtaka nani agombee urais.

    Aidha wajumbe hao wamelaani tabia ya badhi ya Makada wa CCM kuwasingizia wananchi wa maeneo yao kuwa wamewatuma kwenda kwa Lowassa ili kumshawishi atangaze nia ya kugombea urais. Wajumbe hao wamesema watu hao ni maswahiba wa LOWASSA wa siku nyingi na wanafanya hivyo kwa sababu hiyo na siyo kwamba wametumwa na wananchi wao.
     Baadhi ya Makada hao wa CCM na ambao ni maswahiba wa siku nyingi wa LOWASSA ambao wanakwenda kwa LOWASSA kwa madai kuwa wametumwa na Wananchi ni pamoja na Mjumbe wa NEC kutoka Wilaya ya BUSEGA, Dk. RAFAEL CHEGENI na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Serengeti na mjumbe wa NEC.
Lowassa ambaye inasemekana amewateka wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM,NEC ambao wako 260 kati 370 waliopo,wajumbe hao wa Lowassa 260 wameaapa kufa naye.
Kwa Sasa Lowassa amepata pigo kubwa kwenya Nafasi ya Kamati kuu ya CCM,CC ambayo ndio yenye kazi ya kuyachuja majina na kuyarudisha NEC ili wachaguliwe kuwa Viongozi ,pigo limetokana baada ya Mbunge wa Muleba Profesa Anne Tibaiujuka kusimamishwa na CC,kwa madai ya kupokea pesa za Escrow.
Profesa Tibaijuka ambaye alitolewa Kafala na Rais Kikwete kwa kufukuzwa na kwenye Nafasi ya Uwaziri wa Nyumba na Maendeleo na Makazi ili kuwarainisha Wahisani ambao wamegoma kutokana na ufisadi wa Escrow.

Duru za kisiasa zinasema Profesa Tibaijuka ni mtu wa Lowassa kwahiyo kuondolewa kwake katika Nafasi ya cc kunazidi kumpa pengo Waziri huyo aliyejiuzulu kutoka na kubakiwa na wajumbe wa wawili ambao ni Sophia Simba na Sadifa Juma Khamis,kati ya wajumbe zaidi ya 38.

Hakuna maoni