Zinazobamba

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU ACT-TANZANIA SOMA HAPA KUJUA




ACT-TANZANIA
ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY.

TAARIFA KWA UMMA.

Ndugu wananchi
Naomba nichukue fursa Hii kuwashukuru kwa kukipokea chama chetu na tunawaahidi tutasimamia misingi yetu kumi ya chama ili kuweza kuwaletea maandeleo.

Lengo kuu la taarifa hii kwenu nyinyi ambao ni wadau muhimu sana kwa ustawi wa chama chetu ni kutoa taarifa za matukio muhimu ya chama katika kipindi hiki.

Tulianza chaguzi za ndani ya chama tarehe 17/1/2015 kwa kufanya chaguzi za mashina na matawi nchi nzima.
Na pia tulienda na Uchaguzi za kata kuanzia tarehe 8/2/2015 Na kisha chaguzi za majimbo zilifanyika kuanzia tarehe 22/2/2015 na mpaka sasa tumefanikiwa kufanya chaguzi katika majimbo 116 nchi nzima.

Tutaanza kufanya chaguzi katika mikoa kuanzia tarehe 8/3/2015 Na mpaka sasa mikoa 24 imekidhi takwa la kikatiba la kufanya uchaguzi ndani ya chama.

Tutakuwa na mkutano mkuu wa chama tarehe 28/3/2015 na tunategemea kukamilisha yafuatayo katika mkutano huu:-
1.Kupokea taarifa ya kazi za chama tangu 5/5/2014 mpaka 28/3/2015.
2.Marekebisho ya katiba ya chama
3.Na uchaguzi wa chama ngazi ya Taifa katika nafasi zifuatazo:-
a)Kiongozi Mkuu wa Chama
b)Mwenyekiti wa chama Taifa
c)Makamu Mwenyekiti bara
d)Makamu Mwenyekiti Zanzibar.

Aidha Halmashauri kuu ya chama itachagua Katibu Mkuu wa chama Taifa Na pia Kamati Kuu ya chama itachagua Naibu Katibu Mkuu wa Bara na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Tunatoa wito kwa wanachama wetu nchi nzima kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi za kitaifa na muda wa kuchukua fomu ni kuanzia tarehe 15/3/2015 na mwisho wa kurudisha ni tarehe 20/3/2015.

Tarehe 29/3/2015 tutafanya Mkutano Mkuu wa kwanza wa kidemokrasia na uzinduzi rasmi wa chama ambao utafanyika Mkoa wa Dar-es-salaam.

Tunatoa wito kwa wanachama wa ACT-Tanzania nchi nzima na Watanzania kwa ujumla kuhudhuria katika mkutano mkuu wa kidemokrasia.

Utaratibu wa kuhudhuria ni kujisajili kwa makatibu wa majimbo na mikoa wa ACT-Tanzania waliopo nchi nzima mwisho wa kujisajili ni tarehe 16/3/2015,Aidha wote watakaohudhuria watajigharamia usafiri na malazi.

Tunatoa wito kwa wanachama wetu nchi nzima kushiriki chaguzi za ndani ya chama zinazofuatia Na pia kuwaomba wajitokeze kwa wingi katika mkutano mkuu wa kidemokrasia na uzinduzi wa chama wa kihistoria.

Na baada ya uzinduzi kutakuwa na kazi za uenezi wa chama nchi nzima ila tutaanzia na Mikoa ya Arusha ,Mbeya,Kigoma na Mwanza.

Pamoja na salamu za uzalendo ACT-Tanzania Taifa Kwanza.

Imetolewa leo tarehe 5/3/2015
Mohammed Massaga
Naibu Katibu Mkuu Bara.
+255 718 38 88 88.

Hakuna maoni