KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATOA USHAURI MKUBWA TMA, SAKATA LA BIL. 1.5 LAWA GUMZO
Kamati ya kudumu ya Bunge la miundo mbinu Imeitaka serikali kufanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa mamlaka ya hali ya hewa wanapata jengo lao Kwani ilivyo sasa hali si shwari kutokana na ukweli kuwa mabilioni ya shilingi yanatekeketea kwa kulipa pango,
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, baada ya kukamilika kwa matembezi katika mamlka hiyo,Kibona amesema kwa mujibu wa Taarifa ambayo wamesomewa na mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Bi. wakati akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa taasisi yake mapema hii leo Takribani Bilioni 1.5 hutumika kulipa pango la ofisi fedha ambazo ni za mlipa kodi
Amesema fedha hizo zimekuwa zikilipwa toka 2004 mpaka sasa kitu ambacho kama wangekuwa makini wangeweza kujenga Jengo lao wenyewe, na hivyo kujinusuru katika gharama ambazo hazina maana
Wametuambia hapa tayari kiwanja cha kujenga ofisi kiko tayari, lakini mpaka sasa hakuna mipango ya kujenga jengo, hii hakubaliki ni lazima tufanye kitu ili kunusuru fedha za mlala hoi,Aliongeza,
Naye Mkurugenzi mtendaji wa TMA akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mahojianao maalum, aliiambia mtandao huu kuwa fedha hizo zimekuwa zikiongezeka kutokana na mwenendo wa Dola unavyokwenda,
Tulianza kulipa Takribani Milioni 58 kwa mwezi lakini sasa gharama zimeenda juu zaidi baada ya Dola kupanda , hivi sasa tunalipa jumla ya Tsh. Milion 132 kwa mwezi,na hivyo kufanya gharama za mwaka kufikia Takribani Bilioni 1.5
Amesema hizo ni fedha nyingi , lakini ikumbukwe kuwa sisi tunalipa ada kutokana na square meter moja, na humu tunalipia ghorafa tatu ambazo tumezichukua kwa kazi hii ya kutabiri hali ya hewa,nadhani tukipata jengo letu mambo yatakuwa mazuri aliongeza
Hakuna maoni
Chapisha Maoni