WTAALAMU WA LOGISTICS AND TRANSPORT KUKUTANA ARUSHA KUJADILI MATATIZO YA MISONGAMANO NA USAFIRI WA BONGO
Wito umetolewa kwa wadau mbalimbali ambao wanajishughulisha na shuguli za uondoshaji mizigo bandalini na usafirishaji wa mizigo na abiria kujitokeza kwa wingi kuhudhulia mkutano wa kipekee wa wataalam wa logistics and transport management ili waweze kujionea na kujifunza mambo mapya katika sekta hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo, mwenyekiti wa maandalizi wa mkutano huo ambaye pia ni mkuu wa chuo cha Admini and Logistics toka JWTZ, Brigedia Harrison Joseph Mase bo amesema watanzania wanakila sababu kuhudhulia mkutano huo ambao wa kihistoria katika nchii ambayo inakabiliwa na changamoto kubwa za kilogistikia,
Akitaja baadhi ya changamoto ambazo mpaka sasa taifa bado zinapambana nazo kuwa ni pamoja na ongezeko la foleni katikati ya jiji, Ongezeko la mizigo bandarini ambapo mpaka sasa takwimu bado zinaonyesha kuwa kuna magali mengi hayajatoka kutokana na logists mbovu iliyopo sasa,
Masebo ameendelea kusema kuwa siku hiyo wataalam mbalimbali watawasilisha mada kuhusu namna walivyoweza kudhibiti changamoto za kilogistikia hadi kufanikiwa kuondoa tatizo la foleni nchini mwao,na hivyo taifa lao kuweza kuongez kipato kutokana na watu wake kufika katika ofisi zao kwa wakati muafaka na kuondoka kwa wakati muafaka.
Naye kwa Upande wake, Mkuu wa shule ya Anga, ambaye pia ni mwalimu toka chuo cha Usafirishaji, Ndg.Juma Fimbo ameuzungumzia mkutano huo kama fursa pekee kwa makampuni ya usafirishaji na logistics kwenda kujifunza namna ya kuweza kufanya shughuli zao kwa weledi mkubwa tena ulio tukuka,
Fimbo amesema kimsingi bado watanzania hawafahamu kuhusu suala zima la Logistics na hivyo amewataka kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo utakaofanyika huko Arusha katika Hoteli ya Mount meru,
Kwangu mimi Logistics bado haijaweza kutukomboa na hiyo ni kutokana na serikali yenyewe kutoipa kipaumbele wazo hili liweze kushika hatamu, Ukiniuliza leo unadhani tufanye nini ili kupunguza msongamono hapa jijini Daresalaam, kilogistic nitakujibu vizuri tu, lakini kwa kawaida huenda ungesema tupanue barabara zetu, lakini ukweli ni kwamba ukifanya hivyo maana yake ni kuwa unaruhusu watu waendelee kuja mjini na hivyo hata uapanue vipi bado msongamano utakuwepo,
Kubwa ni kutawanya huduma za kijamii pembezoni mwa mji na hivyo itakuwa rahisi kwa trip making kupungua.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni