KAMANDA KOVA AWAPIGA STOP CCM KUFANYA MAANDAMANO DAR
KAMISHINA WA POLISI KANDA MAALUM YA DARESLAAM, AKIFAFANUA JAMBO KWA WAANDISHI WA HABARI. KOVA AMEPIGA STOP MAAANDAMANO YA CCM, HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJI DARESLAAM. |
MAANDAMANO. |
KOVA AMEPIGA MARUFUKU MAANDAMANO KAMA HAYA AKIDAI KUWA YALILENGA KULETA VURUGU JIJI DARESALAAM. |
Kwa mara ya kwanza jeshi la polisi kanda maalum ya Daresalaam, limezuia maandano ya amani yaliyopangwa kufanywa na vijana wa CCM ilala, kutokana na maaandano hayo kuonyesha dalili za kuwa na fujo,
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo ofisini kwake kamanda huyo wa polisi amesema Jeshi lake limewazuia viongozi wa cahamacha mapinduzi mkoa wa ilala kufanya maandano hiyo kesho na hiyo inatokana na ukweli kuwa taarifa za kiiterinjisia kuonyesha wazi dalili za maandamano hayo kutawaliwa na vurugu na hiyo kuwakosesha amani wakazi wa jiji la Dareslaam,
Moja ya sababu kubwa ambayo imewafanya jeshi hilo kuwazuia wanachama hao kufanya maandamano ni kwa sababu maandano hayo yangewahusisha wazee wa bodaboda, mama na baba lishe, pamoja na wafanyabiashara ndogondogo ambao wamejipanga kutumia maandano hayo kutoa dukuduku lao, na kusema kufanya hivyo siyo halali kwani kama kweli wanamatatizo yanayowakela basi wafuate taratibu za kisheria,
Mwanzoni kabisa walipoleta barua yao tuliwakubalia lakini baadae tumepata taarifa kupitia whatsup kwamba madhumuni ya maandamano ya vijana ya ccm yamebadilika kutoka kuazimisha miaka 38 ya uanzishwaji wa chama hicho hadi kuwa maandamano ya kutoa kero za wamachinga, mama lishe na waendesha pikipiki alimaaruf bodaboda,
Hivyo kwa kauli moja jeshi limesimamisha maandamano hayo ambayo yalikuwa na dhamira ya kusheherekea miaka 38 ya chama
Aidha katika hatua nyingine jeshi hilo limesema limepokea taarifa ya ummoja wa vijana wa chadema BAVICHA wakitaka kufanya maandano ya amani kwenda kwa tume ya uchaguzi kuhoji ni lini zoezi la uandikishwaji kwenye daftari la mpiga kura utaanzana na je utaratibu wa wanafunzi wa chuo kikuu ukoje katika suala zima la kupiga kura,
Kova amesema kuhusu barua hiyo jeshi la polisi wamepokea na kwamba taarifa kama maandamano hayo yatakuwepo ama hayatakuwepo watajulisha viongozi wa chama hicho.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni