Zinazobamba

UOZO WAIBULIWA BANDARINI, KUMBE HII NDIYO SABABU YA KUJAA KWA MAKONTENA BANDARINI....


Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Sami Agency Limited ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya chama cha TAFFA Ndg Waheed K Saudin akiteta na waandishi wa habari kuhusu uozo unaoendelea bandarini huku mamlaka zinazohusika zikiwa bado zinasuasua kuchukua hatua zinazostahili ili kumlinda mlaji ambaye ni mwananchi wa kawaida. Mkurugenzi huyo amesema changamoto ambayo wanayo maagenti wote ni tozo za storage ambazo zinalazimishwa kulipwa na watu wa ICD huku wakijua wazi kuwa hiyo ni dhuruma.
Ni kama amefunguka, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Sami Agency Limited ameibuka na kuitaka serikali kuangalia upya suala zima la ,kulipa storage charges ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikiwaumiza wananchi kutokana na ukweli kuwa tozo hiyo ni kama inatengenezwa ili watu wapate kushibisha matumbo yao huku mlala hoi ndio anayeumia zaidi,
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mapema hii leo, Mjumbe huyo toka chama cha Taffa amekili kuwa katika vitu ambavyo serikali inapaswa kuingalia kwa sasa huko bandarini basi ni sekta hiyo ya uondoshaji wa mizigo kwani hivi sasa kumejaa mizengwe ambayo haina ulazima,
Mkurugenzi huyo ameendelea kufunguka kuwa, sakata la storage charges limekuwa ni kero kubwa sana kwa maagent wote na hiyo inatokana na ukweli kuwa tozo hizo zinalipwa ili kujaza matumbo ya watu binafsi
Ngd mwandishi hivi sasa tunachangamoto ya kulipa storage charges, Chaji hii ni kama ya wizi kwani kwa mujibu wa sheria baada ya meli kushuka kuna siku saba ambazo agenti anatakiwa kutoa mzigo wake, na ukifanikiwa kutoa ndani ya siku saba basi hutalipa storage chaji,
Cha ajabu ni kwamba hata kama meli imefika kwa wakati agenti haruhusiwi kutoa mzigo mpaka ICD waufikishe katika yadi zao, na wakiufikisha katika yadi zao ndiyo hapo sasa linakuja suala la storage chaji ambazo ni lazima kuzilipa ili utoe mzigo wako katika yadi yake,
"Kimsingi hatukatai kulipa hizo chaji lakini tunachoomba ni kwamba suala zima la kuhesabu siku za mizigo yao kukaa katika yadi zisianzie mara tu meli inapofika na badala yake hesabu zifanyike baada ya mizigo kufika katika ICD zao" alisema  ndg Saudin

Mjumbe wa bodi ya TAFFA ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni inayojishughulisha na uwakala wa kutoa vitu bandalini( CREARING and fowarding agency, transport, logistics) akifafanua jambo mbele ya kamera ya blog ya jamii kuhusu dhuruma inayofanyika kwa wananchi na watu wenye ICD, hapo anaonyesha baadhi ya BL na DO ambazo huwa tayari kwa muda mrefu lakini ICD wanashindwa kufikisha mizigo kwa wakati.

Amesema suala la kuanza kuhesabu zile siku saba za bure mara tu meli inapofika linajenga picha kuwa watu wa ICD wanacheza mchezo mchafu wa kuchelewesha mizigo bandarini ili waweze kupata faida kubwa, kwani zidi siku zinavyoongezeka ndivyo faida kwa watu wa ICD inavyotengenezwa zaidi,
Ameendelea kusema kuwa katika hilo agenti haumii lakini anayeumia ni mwananchi ambaye ndiyo mtumiaji wa mwisho wa bidhaa husika, kwani gharama zote zitaweka katika bidhaa ambayo mtumiaji atapaswa kuinunua kwa vyovyote vile

Aidha katika hatua nyingine mtaalam huyo wa kuondoa mizigo bandarini ameufurahia mfumo mpya wa TANSIS ambao amesema ni mfumo mzuri ambao umewaka uwazi kwa wateja pamoja na TRA,
Amesema mwanzoni kulikuwa  na mazingira ya kutokuwa na uwazi katika kuondoa bidhaa bandarini lakini mfumo huo wa sasa umekuja kujibu matatizo yote ambayo yalikuwa yanawakwaza wateja wao,
 

Hakuna maoni