IRAN WAKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA KITANZANIA, WATOBOA SIRI YA KUPATA SOKO NCHINI IRANI
Mkurugenzi mkuu toka wizara ya mambo ya nje ya ilani anayeshughulikia biashara kwa nchi za Afirika, (anaehojiwa)akifafanua jambo kuhusu fursa za ilani ambazo wafanyabiashara wanatakiwa kuzikimbilia |
Fursa sasa zimefunguliwa, Ubalozi wa Iran hapa nchini
umefungua milango kwa wafanyabiashara wa kitanzania kuanza kupeleka bidhaa zao
katika soko la nchini humo ili kuweza kujiongezea kipato kutoka taifa hilo,
Akizungumza katika
mkutano maalum uliowakutanisha wafanyabiashara wa kitanzania na wa nchini
Ilani, Mkurugenzi wa biashara kwa Afrika toka wizara ya mambo ya nje ya Ilan, amesema fursa
kwa taifa hilo zipo kubwa, cha msingi ni wafanyabiashara wa kitanzania
kuchangamkia fursa zilizopo ili waweze kuongeza biashara zao kuuzwa nje ya nchi
na hivyo kuweza kuliletea taifa faida za kiuchumi,
Akizungumza na mtandao huu, rais wa TCCIA hapa nchini, amesema Watanzania wanatakiwa kuchangamkia fursa za kibiashara ambazo zinapatikana katika Taifa la Irani,
Katika hatua nyingine, Rias huyo amezungumzia kushindwa kwa taifa la Tanzania kutumia fursa za soko La AGOA na kusemakuwa sababu kubwa ilikuwa ni taifa kutojipanga kuhakikisha tunatumia fursa ambazo zilitangwa ,
Tanzania hatuna mtu wa kumlaumu, tutajilaum wenyewe kwani soko la AGOA liko wazi tatizo sisi wenyewe tumeshindwa kujioganize ili tuweze kupeleka bidhaa zetu kama taifa,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni