Zinazobamba

UKEKETAJI BADO NI TATIZO SUGU TANZANIA, WANAHARAKATI WALIA NA SERIKALI


Mwanaharakati ambaye pia ni mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadam Harold Sungusia akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari,Sungusia amesema vitendo vya ukeketaji kwa hapa nchini vimeendelea kukua kwa kasi mno hususani kanda ya kati na kuongeza kuwa vitendo hivyo  vimebuniwa mbinu mpya ambayo sasa vimehamia kwa watoto wa dogo ambao hukeketwa baada ya kufikisha miezi mitatu


Mkurugenzi wa uwajibikaji na uwezeshaji Imelda Urio akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu siku ya kupinga ukeketaji Iliyoazimisha hii leo,Imelda hakusita kuonyesha masikitiko yake juu ya kuongezeka kwa vitendo vya ukeketaji japo kuwa kunanguvu kubwa inafanywa na wanaharakati ili kutokomeza vitendo hivyo.
Licha ya jitihada ambazo mashirika mbalimbali yamekuwa yakifanya kuhakikisha vitendo vya ukeketaji vinatoweka katika ardhi ya Tanznia, bado nguvu hiyo imeeonekana kutofaa chochote kwani mpaka hivi sasa vitendo hivyo ndiyo kwanza vimeongezeka kwa kasi ya ajabu,

Akizungumza na vyombo vya habari mapema hii leo, Mwanasheria wa kituo cha sheria na haki za binadam, Bwana Harold Sungusia hakusita kuonyesha masikitiko yake kutokana na kuona vitendo vya ukeketaji sasa vikiongezeka kwa kasi huku mbinu mpya zikiibuliwa ili kukwepa mkono wa sheria

Amesema japo mashirika mbalimbali kama TAWLA, TAMWA,DIAC, CCT, WORLD VISION TANZANIA,NAFGEM, AFNET, WOWAP, CDF, WLAC yakitumia muda wao mwingi kuelimisha umma juu ya madhala ya kuwepo kwa vitendo vya ukeketaji lakini bado mafanikio mpaka sasa hajaonekana zaidi ya vitendo hivyo kuongezeka.

"Ni kama tunatwanga maji kwenye kinu, faida yake ni kulowana, tunachoona hapa ni serikali sasa ikatae vitendo hivi ndipo hapo tutakaposhinda vita hii ya ukeketaji," Aliongeza Sungusia

Anasema ukiangalia sheria yetu ya nchi iko wazi kabisa kuwa vitendo vya ukeketaji ni makosa ya jinai na hii ni kutokana na sheria ya kanuni ya adhabu ya  mwaka 2012 kifungu cha 169A (1) Kinachoainisha kuwa ukeketaji ni ukatili dhidi ya watoto

Naye kwa upande wake, mwanasheria Imelda Urio amekiri waziwazi kuwa jitihada za kuondoa ukeketaji hapa bongo lazima mbinu zingine zianze kutumika hasa serikali lazima ione umuhimu wa kuzuia vitendo hivi ambavyo vinawathiri watoto,
Kwa takwimu zilizopo,mwaka 2014 amabao ulikuwa mwaka wa ukeketaji kwa mujibu wa jamii ambazo zinadumisha mila hii ya ukeketaji , vitendo vya ukeketaji vimeonekana kuongezeka mno ukilinganisha na mikoa mingine,
Kwa mfano kwa wilaya ya Tarime peke yake jumla ya watoto 1400 wamekeketwa na watoto hao ni kutoka koo za  Bukira Watoto 212, Bukenye Watoto 230, Iregi watoto 800, na nyabasi watoto 160. Idadi ambayo inadaiwa ni kubwa sana na inayosikitisha, na kwa wilaya ya Serengeti ni jumla ya watoto 500 wamekeketwa katika mwaka huo.,
Kuhusu mbinu mpya, ni kwamba makabila ambayo yanadumisha mira sasa yameanza kukeketa watoto wao wakiwa na umri mdogo hivyo ni vigumu kwa wanaharakati kugundua idadi halisi ya waliokeketwa na kuwachukulia hatua za kisheria.
mwisho.











Hakuna maoni