Zinazobamba

UTAFITI-HAWA NDIO WAANDISHI WA HABARI BORA WA MAKALA NCHINI,YAELEZWA BILA HAWA MAGAZETI YAO HAYAUZI SOMA HAPA KUJUA

EDSON KAMUKARA

KWA mda miezi mitatu sasa Mtandao huu umefanya utafiti katika sekta ya Habari hususani magazeti ili kutaka kujua ni Waandishi gani wa Habari kwenye magaeti ambao makala zao zinapendwa sana.
           Mtandao huu katika utafiti wake uliangazia magazeti zaidi ya 20 ambayo yamesajiliwa na msajili wa magazeti nchini pamoja na mambo mengine utafiti huo ulijikita zaidi katika kuangalia hamasa za watanzania katika kutaka kuzisoma Makala za waandishi hao.
            Katika utafiti huo walishirikishwa hadi wauza magazeti pamoja na wasomaji wa magazeti.
          Katika Utafiti huo mfupi tunakabaini Wafuatao ni ndio Waandishi watano Bora ambao Makala zao zinasomwa sana nchini Tanzania.
               1..Jenerali Ulimwengu
Huyu ndio miongoni mwa Waandishi wa Makala bora kabisa nchini Tanzania,ambaye anaandika makala ambapo wananchi hawataki hata wiki ipite bila kusoma makala zake.

Ulimwengu 

             Ulimwengu ambaye ni anaandikia makala zake kwenye Gazeti la Raia mwema na Raia Tanzania,katika magazeti hayo amekuwa akiandika makala mbalimbali ikiwemo za Kisiasa pamoja na kijamii,na kufanya Gazeti la Raia Mwema kuwa ni miongoni mwa gazeti linalopendwa zaidi,
             Gazeti la Raia Mwema ni Gazeti linalotoka maramoja kwa Wiki limekuwa likipendwa sana kutokana na mchango anaoufanya mwandishi huyo.
           Ulimwengu makala zilizompa heshima kubwa sana ni –Acha kelele toa hoja,pamoja Hapa kwetu tunakimbilia wapi ,na makala nyingine nyingi.

                  2..Saed Kubenea
Huyu naye ameshika nafasi ya pili ya Waandishi bora wa Makala nchini Tanzania,Kubenea jina lake sio geni sana kwenye masikio ya watanzania kutokana na kazi kubwa anayofanya hapa nchini kwenye sekta ya Habari.
              Kubenea anasifika kutokana na Ujasili aliokuwa nao katika kufichua Maovu ya Serikali pamoja na Vyama vya kisiasa ,mwandishi huyo makala zake nyingi anaandikia kwenye gazeti La Mawio ambalo yeye inasemekana ni Mhariri wa kisili wa Gazeti hilo.
            Kabla ya kuandikia Mawio kubenea pia alikuwepo kwenye Gazeti la lilofungiwa kwa mda usiojulikana la Mwanahalisi.
                Katika gazeti la Mwanahalisi kubenea alikuwa ni mkurugenzi wa gazeti hilo,baada ya kufungiwa gazeti hilo,kubenea hakutaka kipaji chake kupotea cha kuhabalisha watanzania ndipo akajiunga kwenye Gazeti la Mawio.
              Uwepo wa wake kwenye Gazeti hilo la Mawio ndipo amelifanya limekuwa gazeti linalopendwa zaidi sana nchini Tanzania,gazeti la Mawio linatoka mala moja kwa wiki hususani kila alhamisi.
          Kwa Mujibu ya wauza magazeti wanasema katika magazeti yanayofanya Vizuri katika wiki ni gazeti la Mawio lipo.
                 3---Edo Kumwembe.
                  Huyo naye ameshika nafasi ya Tatu kati ya Waandishi wa Habari ambao wanaandika makala zinazopendwa zaidi.
               Kumwembe,ambaye ni tofauti na Ulimwengu,kubenea kwani Kumwembe yeye anaandika makala za habari za Michezo kwenye gazeti la Mwanaspoti.
                Kabla ya kuandika mwanaspoti Kumwembe alikuwa anaandika makala kwenye Gazeti la michezo Dimba,ambapo alipokuwa huko kumwembe alisifika sana kwa kuandika makala nzuri zenye kuwafanya wasomaji wasikubali hata wiki kupita bila kusoma makala zake na hata alivyohamia Mwanaspoti huko ndipo alipozidi kupata umaharafu sana kwa makala zake zenye ubora.
              Kitu kinanchomtofautisha kumwembe na waandishi wengine wa makala za michezo kumwembe amekuwa mtu anayefanya utafiti kabla ya kuandika makala zake ikiwemo hata kwenda hata nchi za nje husani Amerika na Ulaya huko walipo wachezaji nyota wa mpira wa miguu kupata taarifa zaidi.
            4—Edson Kamukara
             Huyu naye ameshika nafasi ya Nne kati ya Waandishi wa Habari wanaoandika makala zinazowafanya wasomaji wazipende zaidi.
           Edsoni Kamukara ambaye anatoka kwenye Gazeti la kila siku la Tanzania Daima, naye anasifika sana kwa kuandika makala zenye kupendwa zaidi amekuwa akiandika makala bila ya uoga wowote.
               Kamukara ambaye pia ni Mhariri wa Gazeti la Jumatano la Tanzania daima ,amekuwa akiandika makala zenye kutoa elimu pamoja na kuwakosoa vongozi walioko Makadarani  ambao wanakwenda kinyume.
          Umakini wa Msomi huyo wa Masula ya habari kutoa chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino amelifanya Gazeti la Tanzania Daima kuwa ni miongoni mwa magazeti linalotoka kila siku linalopendwa zaidi.
Jabir Idrissa
                     5---Jabir Idrissa
                 Huyo naye ameshika nafasi ya Tano kati ya Waandishi wanaongoza kwa undikaji wa Makala zinazowafanya wasomaji walipende Gazeti kulisoma kila siku.
           Jabir ambaye anatoka kwenye gazeti la Mawio naye amekuwa ni miongoni mwa Waandishi wanaongoza kwa uandishi makini wa Habari pamoja na Makala zenye kuifanya Jamii ilipende kusoma gazeti hilo.
  

Hakuna maoni