HABARI ILIYOTIKISA JIJI-NAHODHA AJITOSA URAIS 2015 CCM,ASEMA ATAPAMBANA KUFA NA KUPONA SOMA HAPA
NA KAROLI
VINSENT
HUKU zikiwa zimebaki wiki chache Kabla ya chama
cha Mapinduzi CCM akijapuliza Kipenga ili kuashiria kuanza kwa kampeni za
makada wake kuwania nafasi ya Urais ili kumrithi Rais anayemaliza mda wake
Jakaya Kikwete,sasa Kada mwingine wa chama hicho Shamsi Vuai Nahodha
amejitokeza na kuitaka nafasi ya hiyo ya Juu ya nchi kwenye uchaguzi wa mwaka
2015.
Kuibuka huko Waziri huyo wazamani wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa,kumekuja wiki moja tangu Rais Jakaya kikwete kusema kwenye Sherehe za
miaka 38 ya CCM yalifonyika mkoani
Songea na kuwataka wananchi washawishi makada wengine wenye sifa wajitokeze
kwenye nafasi ya Urais na kuongeza mgombea atakayerithi mikoba yake bado
ajajitokeza.
Nahodha ambaye aliwaikuwa kiongozi wa juu
huko Zanzibar ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na
FULLHABARI.BLOGS ambapo pamoja na mambo mengine alisema kwa sasa yeye anaitaka nafasi
hiyo ya urais kwenye uchaguzi mwaka 2015 ndani ya chama hicho, kwa kujinadi
naye anafanya kimya kimya,kwani amebaini anazo sifa zote.
“kiukweli mimi ninazo sifa zote za kuwa kuiongoza Tanzania katika miaka 10 ijayo, kwani ninasifa zote,nimekuwa muadilifu
sana, tena ni kiongozi mwenye uwezo,nakuhakishia rasmi najitosa na mimi kwenye
kupambana na wengine waliojitokeza”alisema Nahoza.
Nahoza aliongeza kuwa uzoefu
aliokuwa nao katika kuongoza nafasi nyeti ya wizara ya ulinzi na kusema unampa
imani ya kuweza kuwatumikia wananchi.
“Mimi ni kuongozi mzoefu
wa masuala ya ulinzi,nimeongoza wizara ya ulinzi bila matatizo yeyote na
nakuhakikishia hata ukienda kwa wanajeshi wote wanatakwambia mimi ni mtu gani,”aliongeza
Nahodha.
Alipoulizwa amejiapanga vipi kupambana
makada wenzake wa Chama hicho wanaotumi pesa na wamejiapiza kufa na kupona ili
kushika nafasi hiyo anayoitaka ili wapate nafasi hiyo alisema “Kiukweli
nakuhahakishia kutangaza nafasi hii naingia kwenye mapambano makubwa naimani
nitafanikiwa na historia yangu inaniruhusu kushindana nao”
Kuibuka huko kwa
Nahonda kunaongeza idadi ya makada ndani ya Chama hicho wanaowania Urais baada
yaWaziri wa Maliasili Lazoro Nyalandu, Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge wa
Nzega, Dk Hamis Kigwangalla na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyesema ametangaza
nia kimyakimya.
Mbali na hao
waliotangaza nia, wapo wanasiasa ambao wamekuwa wakitajwa kuwa miongoni mwa
wanaotaka nafasi hiyo ambao ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Samuel Sitta, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya.
Wapo pia Mbunge wa Songea Mjini, Dk
Emmanuel Nchimbi, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano, Dk Mohamed Gharib Bilal na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk
Asha - Rose Migiro
Hakuna maoni
Chapisha Maoni