HABARI KUBWA-KIKWETE ANYWEA,MAHAKAMA YA KADHI KWISHA,HAWAOGOPA WAKIRISTO,SOMA HAPA KUJUA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Jakaya Kikwete akitafakari jambo
Rais Kikwete anywea, Mahakama ya Kadhi
yaota mbawa
MAHAKAMA ya Kadhi
imeota mbawa. Muswaada uliopangwa kuwasilishwa bungeni leo, tayari umeondolewa
na mjadala wake kufungwa. Anaandika Saed Kubenea… (endelea).
Kuondolewa kwa Muswaada wa Mahakama ya
Kadhi, kumefuatia shinikizo la viongozi wa madhehebu ya Kikiristo, “wanaoungwa
mkono chini kwa chini na Chama Cha Mapinduzi (CCM),” anaeleza mtoa taarifa
ndani ya Baraza la Mawaziri.
Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliodhinisha kuondolewa kwa muswaada
ulifanyika mjini Dodoma jana, chini ya mwenyekiti wake, Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete.
Taarifa kutoka ndani ya kikao cha
baraza la mawaziri zinasema, kuondolewa kwa muswada kumetokana na hofu kuwa
“kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi, kutawakasirisha Wakristo.”
“Muswaada huu umepigwa chini kutokana
na shinikizo la waamini wa madhehebu ya Kikristo. Hii ni kwa sababu, CCM tokea
awali walikuwa wanapinga kuwapo kwa mahakama hii. Lakini walifanya hivyo
kimyakimya kwa kuhofia hasira za Waislamu,” anaeleza mtoa taarifa.
Kwa mujibu wa andishi
kutoka ndani ya chama hicho la 27 Januari 2015, lililobeba kichwa
cha maneno, “taarifa muhimu za magazeti,” chama hicho kinasema msimamo wa
“madhehebu ya kikirsto unapaswa kuungwa mkono na jumuiya nyingine za kidini.”
Andishi linasema, “Lakini CCM
isijiingize waziwazi ili kuepusha hasira na chuki za kisiasa dhidi yake kutoka
kwa waumini na wafuasi wa madhehebu ya kiislamu nchini.”
Habari kwamba muswaada
huu umeondolewa bungeni, zimepatikana, huku viongozi wa madhehebu ya Kiislamu
– Masheikh, Waalimu na Wanawazuoni – wakiwa wameupinga kambi mjini
Dodoma, kusbiri wanachoita, “ujio wa Mahakama ya Kadhi.”
Hata hivyo, katika hali ambayo
imeacha wengi midomo wazi, hadi Ijumaa mchana, serikali ilikuwa bado haijaeleza
waumini hao wa Kiislamu kuwa imeuondoa muswaada huo bungeni.
Kwa mujibu wa nadishi la CCM, chama
hicho kinasema,
“Katika hali hiyo, CCM
kinaweza kucheza siasa za chini kwa chini, tena kwa siri kubwa, za kuwatumia
maaskofu kutoka jumuiya na taasisi mbalimbali za kidini nje ya uislamu,
kuupinga muswada huo.”
Andishi linasema, “Hii ni kwa sababu,
muswaada huu, ukipitishwa na viongozi wa dini za kikristo wakachukia, ‘sumu’
yao kisiasa ni mbaya zaidi kuliko ya viongozi wa kiislamu.”
Chanzo ni Gazeti la Mwanahalisi.online
Hakuna maoni
Chapisha Maoni