Zinazobamba

NI MUNGU TU ATAKAYEMUOKOA MBOWE,JIMBO LA HAI KULIPOTEZA,MGOMBEA WA CCM,AMTAKA ARUDI KUWA DJ,SOMA HAPA KUJUA


Ni miezi michache imesalia kabla ya Tanzania kuingia katika zoezi nzito sana la uchaguzi mkuu wa Rais Wabunge na madiwani ambapo Tanzania inatarajia kupata Rais mpya kabisa.
           Wakati tukisubiri kwa hamu kubwa kuona ni nani atachukua kijiti cha rais aliyeko madarakani tayari watu mbalimbali wameanza kuonyeha nia ya kukitaka kiti hicho ambapo tumeshughudia watu mbalimbali wakitangaza nia wazi wazi kuwa wanaitaji nafasi hiyo kwa hudi na uvumba huku wengine wakifanya mambo yao kimya kimya ila lengo ni kupata nafasi ya kugombea na hatimaye kupata nafasi ya kuwa rais watanzania.
         Pamoja na nafasi hiyo kubwa ya urais pia majimbo ya uchaguzi nayo yapo katika purukushani kuhakikisha yananyakuliwa na wengine wakifanya kila liwezekanalo kulinda nafasi zao za ubunge katika majimbo yao.
           Moja kati ya jimbo ambalo sasa limeanza kupiganiwa ni jimbo analoongoza mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo chadema ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA mh FREMAN MBOWE ambapo vijana kadhaa kutoka chama cha mapinduzi CCM wameanza kuonyesha nia mbalimbali za kutaka kumngoa mbunge wa jimbo la hai katika nafasi yake hiyo.
http://www.thecitizen.co.tz/…/-/ma…/600/-/32ppvv/-/mbowe.gif
          Katika pitapita za mtandao huu katika mitandao mbalilimbali tumeshughudia kijana ambaye amekuwa akitangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la hai kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM katika uchaguzi ujao huku akiwa tayari anasambaza mabango katika mitandao kana kwamba ni muda wa kampeni la yote hii ni mwendelezo wa kutangaza nia.rejea picha ya juu.
         Katika uchaguzi wa mwaka huu unatabiriwa kuwa na ushindani wa aina yake kutokana na watu kujiandaa kwa kina kuakikisha kuwa wanaangoa watu katika majimbo yake lakini wabunge nao kupigania nafasi zao za kuyaongoza majimbo yao kwa miaka mingine mitano.
Mtandao huu utakuwa ukikupa kila kinachojiri katika harakati hizi za uchaguzi mwanzo

Hakuna maoni