Mshambuliaji wa zamani wa FC
Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi Patrick Kluivert alizungumzia ujio wa
magwiji FC Barcelona nchini mwezi wa tatu mbele ya waandishi wa habari kwenye
mgahawa wa Sports Lounge uliopo jijini Dar Es Salaam ,Pembeni ya Kluivert ni
mwenyekiti wa DRFA Ndugu Almas Kasongo. Magwiji hao wa Barcelona wanataraji
kucheza na wachezaji nyota wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa mnamo mwezi wa
machi tarehe 28.
Mwenyekiti
wa chama cha soka mkoa wa Dar Es Salaam,Almasi Kasongo akizungumza kwenye
mkutano huo katikati na mwakilishi wa FC Barcelona pamoja na Mwakilishi wa
kampuni ya Prime Time Promotions Stuart Kambona ambao ni waratibu wa mchezo huo. Baadhi
ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo mapema leo asubuhi Timu ya wachezaji nyota wa
zamani wa Barcelona FC watacheza na wachezaji wa zamani wa Tanzania, Tanzania
All Stars Machi 28 kwenye uwanja wa Taifa jijini.Mwakilishi wa wachezaji wa
zamani wa Barcelona, Patrick Kluivert alisema jana kuwa mechi hiyo itawahusisha
wachezaji nyota wa Barcelona wakiwemo, Edgar Davids, Gaiza Mandieta, Ludovic
Giuly, Francesco Coco na wengine wengi waliopitia klabu hiyo kwa miaka
tofauti.Kluivert alisema kuwa kikosi chao kina wachezaji nyota ambao ni maarufu
duniani na wanaamini mechi itakuwa nzuri na yenye ushindani mkubwa. Alisema kuwa yeye ni
mwenyeji sana hapa Tanzania kwani huu ni ujio wake wa tatu na anaamini kuwa
jinsi mashabiki wanapenda sana mpira wa miguu, itakuwa fursa kubwa kwao kuona
vipaji vya zamani ambavyo vimetukuka.“Ninafurahi kuja nchini
Tanzania kwa mara ya tatu, ni faraja kubwa pia kucheza hapa nchini kwa mara ya
kwanza, naomba mashabiki wa soka wajae uwanjani kuona mpira wenye ushindani,”
alisema Kluivert.
Mwakilishi wa kampuni ya
Prime Time Promotion inayoratibu mechi na ziara ya timu hiyo ya Barcelona,
Stuart Kambona alisema kuwa madhumuni ya mchezo huo ni kudumisha mahusiano ya
kibiashara ya mpira wa miguu baina ya Tanzania na Hispania, kutangaza utalii na
kuendeleza mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili. Kambona alisema kuwa pamoja
na kucheza soka siku hiyo, ujio wao pia utaitangaza nchi nje ya mipaka yake na
kuleta fursa nyingi hapa nchini.“Wachezaji wa Barcelona wanataingia nchini siku
mbili kabla ya mechi na watakuwa zaidi ya 20, majina ya wachezaji wengine
yatatangazwa baadaye, ila tunaomba wadhamini wajitokeze kufanikisha na
kufaidika na mechi hiyo,” alisema Kambona.
TIMU YA BARCELONA KUTINGA BONGO,NI JEURI YA RUGE WA CLOUDS REDIOA SOMA HAPA KUJUA
Reviewed by Full habari Digital
on
17:47:00
Rating: 5
Hakuna maoni
Chapisha Maoni