HABARI KUBWA LEO.NECTA YATANGAZA MATOKEA.WATU WAFAHULU KINYAMA,SOMA HAPA KUJUA
Katibu mkuu wa baraza la Mitihani nchini NECT Docta CHARLES MSONDE akizungumza na vyombo mbalimbali vya Habari leo jijini hapa |
BARAZA la mitihani Tanzania NECTA leo mapema limetangaza matokeo ya
mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana,matokeo ambayo yaonyesha kuwa
ufaulu nchini umeongezaka kwa asilimia 12.67 ambayio ni kutoka asilimia
57.09,ya mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 69.76 ya mwaka 2014 Inaandikwa na
KAROLI VINSENT NA EXAUDI MTEI Endelea nayo.
Akizungumza na wanahabari mapema leo mesema kuwa kupanda kwa kiwango hicho hicho
cha ufaulu wa mitihani ni matokeo ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali
katika kuboresha elimu nchini kupitia mpango wake wa matokeo makubwa
sasa,pamoja na mpango wa serikali wa kuimarisha tathmini ya elimu katika
mitihani ya kidato cha pili.
Katika matokeo hayo yanaonyesha kuwa jumla ya
watahiniwa 196,805 sawa na asilimia 68.33 walifanya mtihani wa kidato cha nne
2014 wamefaulu huku wasichana wakiwa ni 89,845 sawa na asilimia 66.61 wakati
wavulana waliofaulu ni 106,960 sawa na asilimia 69.85.
Watahiniwa wa shule waliofaulu ni 167643 sawa na
asilimia 69.76 ya waliofanya mtihani,huku idadi ya wanafunzi wa kujitegemea
waliofaulu ni 29,162 sawa na asilimia 61.693 ambapo mwaka 2013 jumla ya
watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 34,075 sawa na asilimia 66.23.
Aidha pia jumla ya watahiniwa wa mihani wa maarifa
yani QT waliofaulu ni 6810 sawa na asilimia 55.29 tofauti na mwaka jana ambapo
jumla ya waliofaulu ilikuwa 6529 sawa na asilimia 43.38.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni